Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na
wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi katika hafla ya kumkaribisha
nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM, iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo
Mkoa wa Pwani.
wananchi
na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mwenyekiti Mstaafu wa
Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete katika hafla ya kumkaribisha
nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM, iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo.
Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu
Dkt. Jakaya Kikwete, mama Salma Kikwete, katika hafla ya kumkaribisha
nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM, iliyofanyika wilayani
Bagamoyo, wengine ni wabunge wa mkoa huo wakimsalimia Mwenyekiti huyo
mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi mbalimbili wa mkoa wa Pwani. (Picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Na David John Pwani
MWENYEKITI
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete amesema
anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama
tulii kabisa.
Amesema
kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo
ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi
nakudai kuwa amejisikia flaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.
Amesema
wakati akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake
Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa
kwenye Komputa.
Dkt.Kikwete
ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha
Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.
Alisema.anashukuru
Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na kwamba amemaliza salama na
ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.
Akikumbuka mchakato wa mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo
mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .
“Ilikuwa
Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye
uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi”amesema Dkt.Kikwete .Aidha amesema
kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa
na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.
Alisema
kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma
maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule
huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani
pale alipojalibu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi
wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.
Aidha
Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa barabara
hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita,
Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi
kufikia wabunge kulumbana.
Amesema
hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa Bahati nzuri
amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku
akitaka watanzania kumuunga mkono.
Wanachana
Wanachama
wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo wamejitokeza Kwa wingi
kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Dkt.Jakaya
Kikwete katika sherehe zilizofanyika wilayani Bagamoyo. Wanachama hao
ambao walitoka katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga
walimuaga na kumkaribisha Kwa nyimbo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269