.

ABIRIA 282 NA WAHUDUMU 18 WA NDEGEYA EMIRATES WANUSURIKA KIFO, NI BAADA YA NDEGE KUWAKA MOTO BAADA YA KUTUA HUKO DUBAI

Aug 3, 2016


NA K-VIS MEDIA NAMASHIRIKA YA HABARI
Shughuli  zote kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Himarati, zimesimama baada ya ndege iliyobeba abiria 300, kupata hitilafu ilipotua na kisha kuwaka moto
Ndeg hiyo Emirates Boeng 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Thiruvananthapuram nchini India wakati ilipokumbwa na mkasa huo mapema leo Agosti 3, 2016.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, abiria wote 282 na wahudumu wa ndege 18 wa ndege hiyo chapa EK521 waliokolewa na wako salama ukiachilia mbali mishtuko kutokanana dhahma hiyo.
Mamlaka za Dubai hazijatoa maelezo zaidi kuhusiana na ajali hiyo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª