Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga
(Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc
Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi
nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano
baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya nchi hizi
mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za pole
kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi
karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti,
2016.
Wajumbe
waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia
ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo
wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha nao
wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga na mgeni wake Waziri Ayrault wakiwa katika picha ya pamoja.
Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Ayrault mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269