Breaking News

Your Ad Spot

Aug 3, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UTURUKI, MWAKILISHI UNHCR NCHINI.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini, Yasemin Eralp masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (katikati) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya.Viongozi hao walijadiliana masuala mbalimbali jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages