Mkurugenzi
Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li (wa
pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
msanii Ali Kiba ambaye atakuwepo kutumbuiza na kutoka kulia ni Msanii
Madee pamoja na Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio
wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC
FESTIVAL.
Msanii
wa muziki wa bongo flava Ali Kiba (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea
miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku
ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini
Dar es Salaam. Wakimsikiliza kwa makini kulia ni Msaidizi wa Masoko na
Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li na kushoto ni Meneja wa
chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu
wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii
wa bongo flava kutoka kundi la TipTop Connenction lenye maskani yake
Manzese, Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio
wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC
FESTIVAL.
Msanii
wa kizazi kipya Bi. Snura alimaarufu ‘Mama Majanga’ akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la
kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes
litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya
Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msanii Madee wa
kundi la Tip Top Connection.
Msanii
wa muziki wa singeli Eskide akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya
chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi
Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian.
Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la
SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Meneja
wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la
kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes
litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya
Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL. Kulia ni
Msanii Ali Kiba.
Kutoka
kulia ni Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini
wakuu wa tamasha la StarTimes Kiswahili linalokwenda kwa jina la
SEREBUKA MUSIC FESTIVAL, Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes
Tanzania, Bw. Damien Li, Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba na
Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian wakikata keki
kuashiria uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya
Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016
kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wasanii
wakubwa nchini kulishambulia jukwaa, wakiwemo Ali Kiba, Lady Jaydee,
Yamoto Band, Madee, Juma Nature, Snura, Stamina, Eskide (msanii wa
muziki wa singeli) na bila ya kusahau wakali wa bongo movie pia
watakuwepo.
…………………………………………………………………………………………………..
WASANII
wa muziki wa Bongo Flava Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa
kutumbuiza katika tamasha la kusherehekea miaka miwili tangu kuanzishwa
kwa chaneli ya StarTimes Kiswahili siku ya Jumamosi ya Agosti 13, 2016
katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi Msaidizi wa
Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li amesema kuwa
tamasha hilo linadhamiria kusherehekea kwa pamoja na wateja wao
mafanikio yaliyofikiwa na chaneli ya StarTimes Kiswahili katika
kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya.
“Chaneli
hii mwaka huu mwezi wa Agosti inatimiza miaka miwili tangu kuanzishwa
kwake mnamo Agosti mosi mwaka 2014. Chaneli ya StarTimes Kiswahili
inaonekana katika nchi mbili za Tanzania na Kenya na hivyo kutoa wigo
mpana kwa wasanii na watayarishaji wa vipindi hapa nchini kupata fursa
ya kuonekana maeneo hayo. Vipindi vingi katika chaneli hii huangazia
masuala ya filamu, muziki, burudani, vyakula, mitindo ya maisha na
mavazi pamoja na tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki hususani kwa
nchi hizo mbili ambavyo huwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili.” Alisema
Bw. Li
“Tamasha
hili litahusisha shughuli mbalimbali hususani kuangazia maudhui
yanayopatikana kwenye chaneli ya StarTimes Kiswahili lakini pia
litapambwa na burudani kadhaa kutoka kwa wasanii watakaoalikwa. Siku
hiyo watanzania watawashuhudia wasanii wakubwa wa muziki wa bongo flava
jukwaani kama vile Ali Kiba, Lady Jaydee, Juma Nature, Madee, Yamoto
Band, Snura na Stamina. Pia kutakuwepo na wasanii mashuhuri kutoka
katika tasnia ya bongo movie ambao filamu zao zinaonekana kupitia
chaneli hii kama vile Wema Sepetu, JB, Steve Nyerere na Ray Kigosi.”
Aliongezea Bw. Li
Chaneli
ya StarTimes Kiswahili inapatikana katika visimbuzi vyote viwili vya
StarTimes yaani cha antenna kuazia kifurushi cha NYOTA kwa shilingi
6000/- na cha dishi kuanzia kifurushi cha NYOTA PLUS kwa shilingi 8000/-
kama malipo ya mwezi. Kampuni hiyo inajivunia kuwa ya kipekee nchini
Tanzania kwa kutoa matangazo bora ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo
kila mtu anaweza kuimudu.
“Ningependa
kutoa wito kwa wateja wa StarTimes na watanzania kwa ujumla kujitokeza
kwa wingi katika tamasha hili litakalofanyika siku ya Jumamosi ya Agosti
13 mwaka huu pale viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Tiketi zitapatikana kwa bei ya kawaida kabisa ya kuanzia shilingi 5000/-
na kupatikana katika vituo vitakavyoanza kutangazwa kwa njia
mbalimbali. Tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru watanzania
kwa kuipokea vizuri chaneli hii na kuifanya kuwa chaguo lao kubwa pindi
watazamapo luninga, hivyo naomba wajitokeze kwa wingi.” Alimalizia Bw.
Li
Naye
kwa upande wake msanii wa bongo flava Ali Kiba akizungumza mbele ya
waandishi wa habari amewaahidi makubwa wateja wa StarTimes na watanzania
watakaohudhuria siku hiyo kuwa watapata burudani ya aina yake.
“Kwanza
kabisa ningependa kutoa pongezi za dhati kwa kampuni ya StarTimes kwa
kutambua mchango wa lugha ya Kiswahili na kuikuza miongoni mwa nchi
wanazofanya biashara. Hii ni fursa ya kipekee kwa wasanii na
watayarishaji wa kitanzania kuweza kupanua wigo wa kazi zao na kuweza
kuonekana sehemu zingine. Kusema ukweli hapo awali wakati matangazo ya
dijitali yanaingia nchini sikuweza kuiona fursa hii lakini sasa ninaona
kazi za wasanii wetu zinaonekana na kutambulika kimataifa.” Alisema Ali
Kiba
“Ningependa
kutoa wito kwa StarTimes kupanua wigo zaidi wa chaneli hii ifike katika
nchi zingine za jirani kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Kongo
hata Afrika ya Kusini kwani kuna watanzania kule na waafrika ambao
wanapenda kufahamu lugha ya Kiswahili na tamaduni za waswahili wenyewe.
Na mwisho kabisa ningependa kuwaalika watanzania wote siku hiyo waweze
kuhudhuria kwa wingi kwani tamasha hili ni lao, nawaomba waje kwa wingi
kusherehekea kwa pamoja maudhui mazuri na ya kusisimua yanayopatikana
ndani yake.” Alihitimisha Ali Kiba au King Kiba kama anavyojulikana
miongoni mwa mashabiki wake
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269