Breaking News

Your Ad Spot

Aug 18, 2016

ASKOFU GADI AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.

Askofu Dr. Charles Gadi akiongea na
wanahahabari hawapo pichani kuhusu mkutano wa maombi ya kitaifa wa kumwombea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.maombi hayo
yatafanyika geita hivi karibuni

Na
Sheila Simba,Maelezo
Askofu
Dkt Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli,katika
mchakato wake wa kuamishia serikali makao Makuu ya nchi Mkoani Dodoma kwani ni
uamuzi wa kijasiri na upaswa kuungwa mkono.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini dare Es Salaam Askofu Gadi amesema kuwa jitihada
zinazofanywa na Rais magufuli ni kubwa kwani jitahada zinaonekana wazi za
kuimarisha mji wa Dodoma na ili uweze kutumika kama makao makuu ya nchi.
‘’Serikali
inafanya kazi nzuri kinachotakiwa ni kumtia moyo Rias wetu ili jambo ili
lifanikiwe na kuhamisha serikali ili kutimiza mpango wa muda mrefu wa kuhamisha
serikali kutoka Dar es Salaam na kwenda Dodoma’’alifafanua askofu Gadi
Aidha
amesema Serikali imejipanga na inaandaa mazingira mazuri kwa watumishi wake
watakao hamia huko kupata mahitaji yote muhimu wanayohitaji,na kuongeza kuwa
jambo hilo litaharakisha maendeleo katika mikoa jirani na Dodoma.
Ameongeza
kuwa imekua ni kawaida ya baadhi ya watu kulalamika kila linapotokea jambo bila
kusikiliza na kufatilia jambo hilo kwa makini,amewaomba watanzania wasiwe watu
wakulalamika kulaumu na badala yake wawe watu wakusiliza na kufata maelekezo.
Ameongezea
kuwa watafanya maombi ya kumuombea  Rais
John Magufuli na viongozi wa serikali katika mji wa buselesele wilaya ya chato
mkoani Geita agosti 25 mwaka huu,kuombea mvua,amani,upendo na mshikamano baina
ya serikali na wananchi wake.
‘’Maombi
haya ni ya kumuomba Mungu alifanye taifa letu kuwa taifa bora kwa uchumi,astawi
wa watuwake na linaloongoza kwa amani na mafanikio katika kila sekta ‘’alifafanua
Askofu Gadi.
Mwisho.



No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages