Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (kulia), akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga,
baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja katika chuo cha
udereva cha Nyato's kilichopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar
es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni walemavu walihitimu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga, akiangalia alama ya usalama barabarani.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati
ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama
barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati
ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram
na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama
barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Mkurugenzi
wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani
nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero, akitoa neno
kwenye mkutano huo.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira
Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
WATU
Jamii ya walemavu ambao ni maderava wa vyombo vya moto wametakiwa
kujitokeza kwenye shule mbalimbali za udereva ili kupata mafunzo ya
udereva ikiwa pamoja na kupata leseni kabla ya kutumia vyombo hivyo.
Wito
huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa
kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19
ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja katika shule ya udereva ya Nyato's
iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala.
Alisema
kuwa ipo haja ya walemavu ambao wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha
vyombo hivyo kabla hawajaingia barabarani ni vema wakapata mafunzo ya
kujuwa alama,kanuni na sheria za usalama barabarani.
"Ni
muhimu kwa kundi hili ambalo leo mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya
udereva kwenda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata fursa ya
kupata mafunzo kama nyie kwenda kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo
vya udereva ikiwamo chuo hiki cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa
kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya
Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu."alisema Mashishanga
Aidha
aliwaeleza wahitimu hao kuwa wahakikishe wanakwenda kupata majaribio
kwa wa kufunzi wa kikosi cha Usalama barabarani ili wapate leseni
zitakazo wafanya waweze kuendesha vyombo vya vya moto.
Kwaupande
wake Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama
barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema
kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao kwenda kuzingatia sheria za usalama
barabarani ikiwa pamoja na kuvaa kofia ngumu,na kutozidisha abiria.
Naye
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa ushirikiano
uliopo kati ya Jeshi hilo na taasisi yake ambapo pia ametoa ofa ya
kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada
wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.
Nyato
alisema kuwa kimeazisha mpango wa kutoa mafunzo ya udereva kwa
kushirikiana na kamati ya Taifa ya usalama kwa watu wenye ulemavu kwa
lengo la kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269