Breaking News

Your Ad Spot

Aug 31, 2016

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.

Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli za utetezi.

Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010 ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe ruzuku hiyo.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages