.

DAS ILALA, EDWARD MPOGOLO AZINDUA KITABU CHA BAJETI, AKATA KEKI KUNOGESHA MIAKA 16 YA TAASISI YA VIJANA YA TYVA, AWAASA KUANDAA MIPANGO INAYORANDANA NA YA SERIKALI

Aug 6, 2016


OfisaTawala wa wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akiwahutubia Vijana waalikuwa na wanachama wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa hafla maalum ya maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo, iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam. 

Na Bashir Nkoromo

Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, pamoja na mambo mengine, Mpogolo amewaasa Vijana wa Taasisi ya Vijana ya TYVA kuhakikisha mipango yao ya kushirikisha Vijana katika shughuli za kimaendeleo, inaendana na mipango ya serikali ili kuwezesha utekelezwaji usiokinzana.

Amesema, iwapo TYVA itapanga kwenye malengo yao mipango inayotofautiana na ile ya serikali kuhusu maendeleo ya vijana na mengineyo, basi utekelezwaji wake unaweza kuwa siyo rahisi kutokana na kukinzana kwa kuwa malengo ya serikali yatakuwa yanaelekeza vingine wakati na wao wamelenga vingine.


Pia aliwataka vijana wa TYVA na wengine kote nchini kuhakikisha wanailinda amani ya Tanzania kwa gharama na nguvu zao zote, akitahadharisha kwamba, amani ni tunu ambayo ikishapotea si rahisi kurejeshwa.


Ameitaka TYVA na Taasisi ngingine za Vijana popote zilipo, kuhakikisha wanakuwa makini dhidi ya watu wasioitakia mema Tanzania, akisema, wapo ndani na nje ya nchi ambao hutamani sana kuona amani ya Tanzania inapotea au inatetereka kwa namna yoyote, na kibaya zaidi kujaribu kujipenyeza kwa makundi ya vijana ili kufanikisha azima zao mbaya.


"Kitu kingine ninacho waasa wakati Taasisi yenu ya TYVA inatimiza miaka 16 sasa, waelimisheni vijana wenzangu, wajihadhari sana, wasije kutekwa na watu waliopo ndani na nje ya Tanzania ili kuwatumia kuharibu amani ya nchi yetu", alisema Mpogolo.


Baadaye Mpogolo alizindua Kitabu cha Mipangokazi au bajeti ya Taasisi hiyo na kukata keki  kushiria TYVA kutimiza miaka 16 tangu ilipoanzishwa na kuendelea kwa mafanikio kufanya kazi zake katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa. OfisaTawala Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo akizindua mpangokazi au bajeti ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, wakati wa maaldhimisho ya miaka 16 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council Dar es Salaa.. Kushoto ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshale
 Vijana wakiwa wamenyoosha miko yao wakati Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyesimama) alipokuwa akiwapiga tafakuri kuhusu umuhimu wa Amani ya Tanzania, alipozungumza nao wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam. 
 Mhasibu Mkuu wa TYVA Zuleikha Ibrahim, akiwasilisha keki meza kuu kwa ajili ya mgeni rasmi, Osisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia) kuikata, kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya TYVA yaliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam. 
 Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akikata keki kunogesha maadhimisho ya miaka 16 ya Taasisi ya Vijana ya TYVA, yaliyofanyika katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam, leo. Kulia ni Ofisa Vijana mkoa wa Dar es Salaam, Masalida Sephania Njashi na kushoto ni Mhasibu Mkuu TYVA Zukeikha Ibrahim, na wapili ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare
 Keki baada ya kukatwa 
 Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare akimlisha keki Ofisa Vijana Dar es Salaam, Masalida Njashi wakati wa hafla hiyo
 Mpogolo akimlisha keki Mwenyekiti wa TYVA wakati wa hafla hiyo. 
 Mpogolo akimlisha keki Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi ya TYVA, Makwita Abdul wakati wa hafla hiyo
 Mpogolo akimlisha keki Mhasibu Mkuu TYVA Zukeikha Ibrahim wakati wa hafla hiyo 
Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Vijana ya TYVA  mwishoni mwa hafla ya TYVA kutimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake. Kulia ni Ofisa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam. Masalida Njashi na aliyeketi kushoto ni Mwenyekiti wa TYVA Nuria Mshare. Picha zote na Bashir Nkoromo. PICHA KEM-KEM ZA BIRTHDAY HIYO YA TYVA TAFADHALI>>GONGA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช