Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Bibi. Scholastica Kevela wakiwa wameshika Tuzo na
Cheti walivyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo
inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and
Excellence) imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi
ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.
Mwenyekiti wa Yono Auction Mart & Co Ltd Bw.
Stanley Kivela akielezea jambo kuhusu Tuzo ya Almas ya Ubora, Uwajibikaji na
Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality Commitment and Excellence) iliyotolewa
na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa
ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku Tanzania
ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa upande wa
Serikali na Yono Auction Mart kwa upande
wa Sekta binafsi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Yono Auction Mart Bibi. Scholastica Kevela akiwa ameshika Tuzo
waliyopewa kutokana na kutoa huduma kwa viwango na ufanisi.Tuzo hiyo
inajulikana kwa jina la The Diamond Eye Award for Quality Commitment and
Excellence imetolewa tarehe 25, Julai 2016 Jijini Rome Italia na Rais wa Asasi
ya Otherways Management & Consulting ya Paris Ufaransa.
Na Frank Shija, MAELEZO.
|
Serikali
ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali kutokana na
jitihada zake za kurejesha heshima na uadilifu miongoni mwa jamii ya
Watanzania.
Haya
yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd Bw. Stanley J.
Kevela aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo iliyopata leo
Jijini Dar es Salaam.
Kevela
ameseme kuwa wao binafsi kama kampuni inayoaminiwa na Serikali na taasisi zake wanayosababu
ya kuunga jitihada zinazoonyeshwa na Serikali katika kupigania maendeleo ya
watu wake kwa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, ubunifu na ufanisi unaostahili.
“Tunatoa
Tuzo hii muhimu kwetu kwa Mhe. Dkt. Magufuli kama ishara ya kuheshimu mchango
wake katika kuliletea taifa letu maendeleo
na kuhakikisha mambo yanafanywa kwa ufanisi na viwango vyenye ubora wa hali ya juu”. Alisema
Kavela.
Amesema
kuwa tokea Rais Magufuli aingie madarakani mambo mengi yamekuwa yakienda vizuri
hivyo ikiwemo suala la ukusanyaji wa Kodi kazi ambayo wamekuwa wakiisaidia
Serikali kwa muda mrefu sasa.
Aliongeza
kuwa Kampuni yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma
zenye viwango tena kwa uadilifu na uwajibikaji usiotiliwa shaka ndiyo maana
wanamuunga mkono Mhe. Rais kwakuwa naye ni muunini wa falsafa ya uwajibikaji,
uadilifu na ubunifu.
Aidha
Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika kuendeleza jitahada za Serikali katika
kukuza ajira wameajiri zaidi ya vijana 200 ambao wako mtaani wakifanya kazi ya
ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Marts &Co Ltd Bibi.
Scholastica Kevela ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kuiamini Kampuni
hiyo kwa kupata huduma zao zikiwemo wakala wa Udalali wa Mahakama na Ukusanyaji
wa Mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA.
Yono
Auction Mart imekuwa ikifanya kazi na Serikali katika Nyanja mbalimba ikiwemo
ukusanyaji wa Kodi kwa niaba ya TRA, udalali wa Mahakama, Uuzaji wa viwanja vya
Serikali na mambio mengine yanayohusu ukusanyaji wa Kodi za Serikali.
Kampuni
ya Yono Auction Marts &Co Ltd ilipata fursa ya kushiriki katika hafla ya
ugawaji wa Tuzo za Diamondo Eye kutokana na Ubora, Uwajibikaji na Ufanisi (The Diamond Eye Award for Quality
Commitment and Excellence) iliyotolewa tarehe 25 Julai 2016 Jijini Rome,
Italy iliyotolewa na Rais wa Asasi ya Otherways Management & Consulting ya
Paris Ufaransa ambapo takribani nchi 49 dunia zilishiriki mchakato huo huku
Tanzania ikiwakilishwa na taasisi mbili ambazo ni Mamlaka ya Angaa (TCAA) kwa
upande wa Serikali na Yono Auction Mart
kwa upande wa Sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269