Breaking News

Your Ad Spot

Aug 20, 2016

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO YAWAACHILIA HURU WAFUNGWA 24 WA KISIASA

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, imewaachilia huru wafungwa 24 wa kisiasa.
Alexis Thambwe Mwamba, Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari kwamba, serikali ya nchi hiyo imechukua uamuzi wa kuwasamehe na kuwaachilia huru wafungwa 24 wa kisiasa kati ya 26 waliokuwa wakishikiliwa gerezani.
Uamuzi huo umechukuliwa na serikali ya Kinshasa kufuatia mashinikizo ya wapinzani katika nchi hiyo.
Wapinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikuwa wakishinikiza kuachiliwa huru wafungwa 26 wa kisiasa wanaoshikiliwa katika magereza mbalimbali ya nchi hiyo kama sharti lao la kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa.
Moja ya magereza ya Kinshasa
Kuachiliwa wafungwa hao wa kisiasa kumetathminiwa kama juhudi za serikali ya Kinshasa za kupunguza mivutano katika nchi hiyo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ujao.
Uchaguzi wa Rais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Hata hivyo kumekuwa na hati hati juu ya kufanyika uchaguzi huo.
Kambi ya upinzani huko Congo imekuwa ikikataa wito wa kufanya mazungumzo na serikali ikidai kuwa ni mbinu ya Rais Kabila ya kutaka kurefusha kipindi cha kubakia madarakani.  
Kwa mujibu wa katiba ya Congo DR, kila raia anayeshinda kiti cha rais wa nchi anaweza kuongoza vipindi viwili mfululizo. Hata hivyo kuna tetesi kwamba kiongozi wa sasa wa nchi hiyo ambaye alishika hatamu za uongozi mwaka 2001 anataka kugombea kwa mara ya tatu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages