.

NAIBU WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, MWANANYAMALA NA KITUO CHA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA CHA FOREPLAN (T) LIMITED, ILALA BUNGONI JIJINI DAR ES SALAAM ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMKAMATA NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MMILIKI WA KITUO HICHO TABIBU JUMA MWAKA KWA KUKIUKA SHERIA

Aug 5, 2016

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Stella Rwezaura (katikati) mara baada ya kutembelea wodi ya wagonjwa ya Mwaisela mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za zilizozaagaa kwenye mitandao ya kijamii za mgonjwa Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani) aliyelazwa katika wodi hiyo anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell)  kulazwa chini katika wodi hiyo kutelekezwa bila kupatiwa matibabu.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto) akipitia kwa makini jalada (file) la matibabu Bi. Kuluthumu Kasongo (aliyelala kitandani) anayesumbuliwa na ugonjwa wa Seli Mundu (Sicle Cell) kujiridhisha juu ya matibabu yake kufuatia taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii leo kuwa mgonjwa huyo ametelekezwa bila kupatiwa matibabu na kulazwa chini katika wodi hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kushoto) akiwa ameongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi kufuatilia ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya leo jijini Dar es salaam kuangalia ubora wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali hiyo.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Dk. Delila Moshi (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) juu ya huduma za Tiba alipotembelea wodi ya watoto njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akizungumza na akina mama wenye watoto waliokuwa katika wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo.Amewahakikishia akina mama hao kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za Afya katika hospitali zake.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akimsalimia mtoto aliyekuwa amelala na akina mama wenye watoto aliowakuta katika wodi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo kukagua ubora wa huduma za Afya.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiwa nje ya Jengo la Kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo hicho Tabibu Juma Mwaka kuendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia kujitangaza kwenye vyombo vya habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11, 2016 la kumtaka asitishe kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya kisheria vya kumruhusu kutoa tiba nchini. 
 Baadhi ya Wagonjwa waliokutwa wakisubiri  Tiba katika kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia)  akizungumzwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED waliokuwa wakitoa huduma licha ya kituo hicho kupigwa marufuku na Serikali kutoa huduma zake nchini.Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata ndani ya saa 24 na kumfikisha Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka agizo la Serikali na kutoa huduma kinyume cha Sheria.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) kwa pamoja wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la  kuchukua vielelezo kama ushahidi wa  Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) na Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Dk. Itikija Mwanga wakiangalia baadhi ya dawa  zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la  kuchukua vielelezo kama ushahidi wa  Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume na sheria.
 Daftari la lenye orodha ya mahudhurio ya wagonjwa lililokutwa dani ya kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla (kulia) akiongea na waandishi na wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba  Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria. Picha/ARON MSIGWA -MAELEZO.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª