5.55am:Fataki zinawashwa katika uwanja huo
5.50am:Na mwenge wa Olympic uliowasili katika uwanja wa Mariccana unapokezwa aliyekuwa mwanariadha wa mbio za Marathon nchini Brazil Vanderlei Cordeiro de Lima - Ambaye anauwasha mwanga katika uwanja huo ishara ya ufunguzi rasmi ya michezo hiyo.
5.32am:Wimbo wa taifa la Brazil unaimbwa kwa sasa katika ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo
5.20am:Uwanja wa Mariccana ulivyofurika maelefu ya mashabiki
5.15am:Bendera zote zimewekwa pamoja kuonyesha ishara ya umoja uliopita baina ya mataifa mbali mbali duniani yanayoshiriki michezo hiyo
5.05am: Na sasa kikosi cha wanariadha wakimbizi pia kinaingia hapa.Baadhi ya wanariadha hawa walikuwa kule nchini Kenya wakifanya mazoezi tayari kwa maandalizi ya michezo hii.
5.00am:Kikosi cha wanariadha kinaingia kikiongozwa na bingwa katika mchezo wa tenisi Andy Murray
4.55am:Vilevile kuna raia wa Brazil ambao licha ya kushimndwa kuhudushuria ufunguzi wa michezo hiyo waliamua kutafuta eneo la juu kama vile milima ili kushuhudia yanayoendelea.
4.45am: Na sasa ni wanariadha wa Afrika Kusini wanaoingia katika uwanja wa Mariccana
4.35am:Wanariadha wa Jamaica wakipita mbele ya mashabiki.Kumbuka ni taifa hili ambalo lina mwanariadha aliye bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt.
4.30am:Hao wanaoonekana mbele ya mashabiki sasa ni wanamichezo wa taifa dogo la Lesotho lililopo kule Afrika ya Kusini
4.15am:Wachezaji wa Marekani ndio hao wanaingia uwanjani
4.10am:Aliyekuwa mchezaji nambari wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada Caroline Wozniacki ndiye anayebeba bendera ya taifa la Denmark.
4.00am: Eneo la katikati la uwanja wa Mariccana limeanza kujaa wachezaji kutoka mataifa mbali mbali.
3.45am:Mwandishi wa BBC Peter Okwoche amekuwa akizungumza na wakaazi wa Rio ambao wamekuwa wakikongamana katika ukumbi wa Fonzona ili kuangalia sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo .
Marina anasema kuwa kile anachokiona ni kitu ambacho hajawahi kushuhudia maishani mwake.''Sijui iwapo wakati huu ni mzuri wa sisi kuwa na michezo hii ,kwa sababu tuna matatizo mengi.Lakini nahisi nafurahi kuwa hapa ili kushuhudia ikifanyika katika taifa langu.
Sijui iwapo raia wa Brazil wataiunga mkono lakini najua watafurahia,na pengine baadaye tutakuwa na matumaini na taifa letu''.
3.15am:Wanamichezo wa taifa la Australia wakipita mbele ya mashabiki
3.10am:Baadhi ya Mashabikio waliotumia usafiri wa aiana mbali mbali ili kuhakikisha kuwa wanahudhuria sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo.
2.50am:Kikosi cha wanariadha wa Olimpiki kutoka Ugiriki ndio hao wanapita mbele ya mashabiki wanaowapongeza
2.45am:Tayari mataifa yanayoshiriki yameanza kuingia katika uwanja wa Mariccana huku shangwe na nderemo zikipamba hewani.
20.30am:Fataki zilizorushwa katika ufunguzi wa michezo ya Rio2016
2.15am: Usalama uliimarishwa nje ya ukumbi wa ufunguzi wa michezo hiyo katika eneo la Barra huku vikosi vya kijeshi vikisambazwa katika kila eneo la mita 25.msongamno wa magari sio mkubwa usiku huu.Inaonekana kwamba wakaazi wa Rio wanafuatilia ufunguzi katika runinga zao majumbani mwao!
2.10am:Wakati huohuo takriban waandamanji 200 walipiga kambi katika ukumbi wa saens Pena nchini Brazil ili kupinga michezo hiyo,ikiwa ni mita chache kutoka eneo linalofanyiwa sherehe za ufunguzi wa michezo.
Maandamano hayo yalioanza mwendo wa saa nane siku ya ijumaa yalikamilika katika ukumbi huo mwendo wa saa kumi na kuelekea katika uwanja wa Marrica.kulikuwa na ripoti za ghasia katika barabara inayoelekea katika uwanja huo lakini baadaye zilisitishwa na muandamanaji mmoja alijeruhiwa.
2.05am:Takriban mataifa 200 yanashiriki katika michezo hii.Sherehe hizo zimeanza kwa kurushwa kwa fataki huku mashabiki waliotoka katika seshemu mbali mbali za ulimwengu wakifurahia.
2.00am: Ni mbwembwe na furaha za aina mbali mbali katika uwanja wa Mariccana ambapo sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki zimeanza.
Sherehe za Ufunguzi wa michezo ya Rio2016
BBC.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269