Breaking News

Your Ad Spot

Aug 17, 2016

VYUO VIKUU VILIVYOPOKEA FEDHA AMBAZO WANAFUNZI HAWAPO CHUONI VYAPEWA SIKU SABA KUREJESHA FEDHA HIZO

Na: Lilian Lundo na
Sheila Simba - MAELEZO

Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.  Joyce
Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha
fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.

Prof.  Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini Dar es
Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la
uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.

Prof.  Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi
hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81 vilivyopo nchini, Katika utafiti
huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa
kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.

“Mikopo ya Wanafunzi
hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa
kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.

Ameendelea kwa kusema
kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi
cha shilingi 3,857,754,460, kiasi ambacho kinatakiwa kurejeshwa na vyuo ambavyo
wanafunzi hao wamebainika.

Aidha, Prof.  Ndalichako amesema kuwa taarifa hiyo
imekabidhiwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachukulia hatua wale wote
watakaobainika kufanya  udanganyifu na
kusababisha Serikali hasara ya mabilioni ya fedha.




Vile vile Prof.
Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo kuweka mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo
ya wanafunzi yanayotumwa Bodi ya Mikopo
kutokana na vyuo vingi kubainika kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye
matokeo ya wanafunzi ambao hawakufanya mtihani au waliofeli na kuandikiwa
wamefaulu ili waendelee kupata mikopo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages