.

WATAALAMU WA TEHAMA WATAKIWA KUWA NA MAADILI.

Aug 25, 2016


Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani  akiongea na wataalam
wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya
Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora
akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku
moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani  akiongea
na wanahabari  hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo.


Na abushehe Nondo,MAELEZO.

Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameiagiza Tume ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano nchini kuhakikisha wanatengeneza
misingi ya uadilifu wa kitaaluma na misingi hiyo itumike kuwadhibiti wale ambao
wanatumia utaalamu huo kwa nia ovu.

Mhandisi Ngonyani aliyasema hayo  wakati akizindua mkutano wa kwanza ambao
umeandaliwa ma Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa  Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema Mkutano huo una lengo la
kuwakutanisha wataalamu wa TEHAMA kutoka katika sekta za umma na sekta binafsi
ili kuweza kujadiliana ni kwa namna gani taaluma hiyo inavyoweza kutumika zaidi
kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

“Wapo baadhi ya watu wanatumia taaluma
ya TEHAMA kwa manufaa mbalimbali ya kujenga uchumi na maendeleo, lakini wapo
wachache ambao wanatumia utaalamu wao kwa manufaa  binafsi ikiwemo kuwadhalilisha watu wengine
na kuwaibia fedha zao katika mitandao” Alisema Mhandisi Ngonyani.

Alisema Tume hiyo ya Teknolojia ya
Habari na  Mawasiliano inatakiwa  kuja na sheria kali ambazo zitawabana wale
wote ambao wamekua na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya vitendo viovu
badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.

Awali akizungumza katika mkutano
huo,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,
Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora
alisema uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano nchini ni jitihada za makusudi za
serikali  katika kukuza Mawasiliano .

Prof,Kamuzora alisema kuwa tume hiyo
ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na hivyo kuwasihi watendaji
hao kuwaelimisha zaidi wananchi  kujikita
zaidi katika kufuata maadili ya taaluma hiyo ili kulifikisha Taifa katika
mafanikio ya sekta  ya mawasiliano.

Alisema Tume ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana na kukua kwa sekta ya
TEHAMA na kuchochea uzalishaji ,ukuaji wa sekta zingine kiuchumi na usambazaji
wa huduma za jamii.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª