Breaking News

Your Ad Spot

Aug 1, 2016

WAZIRI MKUU KASSSIM MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA KILIMONANENANE MKOANI MOROGORO

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana  tikiti maji wakiwa kwenye meza ya Bwana  Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro( PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. wa tatu Kushoto ni mke wa waziri Mkuu, Mary, wakwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na anae fatia ni Naibu Meya wa Temeke Faisal Hassan .

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane  mjini Morogoro , Kushoto ni mke wa Waziri Mkuu  Mary.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu  wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mke wake Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa katika gereza la Karanga  mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea  banda la Magereza katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo, kulia ni  Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu wa Gereza la  Mtego wa Simba, Oman Msekwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (Kulia kwake) wakitazama bwawa la samaki  na banda la kufugia  bata  wakati alipotembelea banda la Magereza katika monyesho ya  wakulima Nanenane mjini Morogoro 
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na mtambo wa kukaushia mboga hizo  katika  katika maonyesho ya wakulima Nanene nane  mjini Morogoro Agosti 1, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kushoto ni mke wake Mary

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages