Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi baada ya kufanya ukaguzi wa
soko la Kimataifa la Mwanjelwa mkoani Mbeya leo Agosti 9, 2016 ambapo
pamoja na mambo mengine amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali, (CAG), afanye ukaguzi wa gharama za ujenzi wa soko hilo mara
moja. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika Halmashauri ya
Jiji la Mbeya baada ya kuwepo kwa ubadhilifu katika ujenzi wa soko la Kimataifa
la Mwanjelwa.
Waziri
Mkuu ametoa maagizo hay oleo hii Agosti 9, 2016 baada ya kulikagua soko hilo na
kuzungumza na wanancvhi ambapo alisikitishwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika
kujenga soko hilo.
“Naambiwa ujenzi wa soko hili umegharibu
shilingi Bilioni 26 badala ya zile zilizotengwa awali shilingi Bilioni 16, nah
ii ni kutokana na uzembe uzembe tu, hii haikubaliki,” alifoka Waziri Mkuu.
Na wote watakaobainika
kufuja fedha hizi watachukuliwahatua mara moja, alisema Waziri Muu Majaliwa
ambaye alifuatana na mkewe Marry.
Hali kadhalika fedha
shilingi milioni 489 zilizotolewana benki ya CRDB ili kuliendeleza soko hilo,
matumizi yake hayaeleweki na hazijulikanizilifanya kitu gani na kumuagiza mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla kufanya uchunguzi ndani ya siku tatu na kumpagtia
majibu.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko hilo
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko hilo
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko hilo
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua soko hilo
Waziri Mkuu akihutubia wananchi mara baada ya kutembelea soko hilo la kisasa
Waziri Mkuu akihutubia wananchi mara baada ya kutembelea soko hilo la kisasa
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na viongozi wa serikali
kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya
kurejea Dar es salaam Agosti 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.
Harrison Mwakyembe na wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote
Stephene.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269