Breaking News

Your Ad Spot

Aug 30, 2016

WAZIRI NAPE AZINDUA MICHEZO YA UMOJA WA VYAMA VYA WALIMU WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.(PICHA NA LORIETHA LAURENCE WHUSM)


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa  Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha WaalimuTanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.


Rais wa Chama cha  Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba.


Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa   mashindano ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), wa pili kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba, na kushoto ni Katibu kutoka Ofisi ya Uhamiaji wa Ubalozi wa Malawi Bw. Michael Gama.  Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo JijiniDar es Salaam.


Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.


Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages