Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Balozi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shio (katikati) kulia ni Waziri
Mambo ya Njena ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano
wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akijianda na mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika
mchana huu katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Hii ndio
muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha mjini
Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
.............................................................
Mkutano
wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Mkutano
huo wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo Tanzania,
Msumbiji na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo mkutano
huo unahudhuriwa na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama
Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC Organ Troika Summit) na Afrika Kusini
kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa
Asasi hiyo.
Baadhi ya
ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya
ulinzi na usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Madagascar na Lesotho, masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro
pamoja na maombi ya Burundi na Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya
Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Katika
mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi
rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa
Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine
mkutano huo utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa
insha katika jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269