Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZONA BALOZI WACHINA NCHINI LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akimkaribisha Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, kwa ajili ya mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. leo, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China, Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong (kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI Zhuan (katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages