Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
Serikali
imewasilisha Miswada miwili inayohusu Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016 na ule wa Sheria ya Usimamizi wa
Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambayo imesomwa kwa mara ya pili
Bungeni ili ijadiliwe na wabunge.
Awali
akisoma Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali wa mwaka 2016, Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema kuwa madhumuni ya Muswada huo ni
kuanzisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuweka
kisheria majukumu yake.
Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa Muswada huo umezingatia masuala mbalimbali
ikiwemo kuanzishwa kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
pamoja na kuainisha majukumu yake na kuanzisha Bodi ya Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mambo
mengine yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni kubainisha utaratibu wa
uteuzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali, majukumu yake na mamlaka yake,
kuifanya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa maabara ya
rufaa na msemaji wa mwisho wa Serikali katika shughuli za uchunguzi wa
kimaabara wa kikemia, sayansi jinai na vinasaba na Muswada huo
utawwzesha kuwekwa utaratibu wa kusajili, kuratibu na kusimamia maabara
na shughuli zote za maabara za kikemia, sayansi jinai na vinasaba.
Zaidi ya
hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kupitia Muswada huo kitawekwa kifungu
maalum chini ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kitakachogharimiwa na Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vielelezo vya
makosa ya jinai, majanga na masuala mengine yenye maslahi ya taifa ili
kuwezesha utekelezaji wa jukumu hilo kwa ufanisi hali itakayosaidia
utoaji wa haki katika vyombo vya maamuzi na kuleta utengamano katika
jamii.
Aidha,
Muswada wa pili uliowasilishwa unahusu Sheria ya Usimamizi wa
Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016 ambapo maoni na ushauri yaliyotolewa
na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma ya Maendeleo ya Jamii
yaliyosawilishwa na Jasmin Tisekwa (Mb) kwa niaba ya Mwenyekiti wakamati
hiyo Peter Serukamba amesema kuwa Muswada huo utasaidia kutungwa kwa
sheria ambayo italeta tija kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Zaidi ya
hayo, Jasmini amesema kuwa Muswada huo utasaidia wanataaluma ya Kemia
kukabiliana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja kwa kuzingatia
taaluma hiyo kwani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta za
elimu, kilimo, viwanda, sheria, afya, mazingira na jamii kwa ujumla
wake.
Akisoma
maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Waziri Kivuli wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ester Mtiko amepongeza
jitihada zinazofanywa na wataalamu wa kemia katika sekta mbalimbali kwa
kuwa wana wajibu mkubwa kwa maslahi ya taifa kwa ajili ya usalama na
kuendeleza maarifa ya kisayansi. (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269