Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
Lete
Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada
ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa
pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.
Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora.
Washiriki
waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana
Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na
Jackline Kimambo.
Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini. |
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.
Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.
Na Dotto Mwaibale
KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.
KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.
Edward
aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa
wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo
huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda
nafasi ya utanashati.
Akizungumza
wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat
George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo
yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa
ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila
mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.
Katika
shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja
kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.
Shindano
hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd
kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha
na wadhamini wengine.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea
kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua
vipaji vya watoto wa kike.
Shindano
hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi
Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and
Spirits Ltd.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269