Breaking News

Your Ad Spot

Sep 29, 2016

DONDOO ZA HOTUBA YA JPM - JANA SEPT 28, 2016, WAKATI AKIZINDUA NDEGE MBILI MPYA ZA ATCL.

Rais Dk. John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege baada kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.

ZIFUATAZO NI DONDOO ZA HOTUMA YA RAIS DK HOHN MAGUFULI WAKATI AKIZINDUA RASMI NDEGE HIZO

=>Rais Magufuli: Lakini unaweza ukajiuliza, ndege hii imetoka Canada imefika hapa, watu wanasema hazina spidi, ni bajaji.

 =>Rais Magufuli: Ndege hizi hazitumiki tu Tanzania, Marekani wana ndege zaidi ya 40 za aina hii, Misri wanazo-

 =>Rais Magufuli: Ukitaka kujenga uchumi, kuinua utalii, huwezi kufanya kama taifa halina ndege- Rais

 =>Rais Magufuli: Ndege ya Jeti, kutoka Dar hadi Mbeya mafuta ni milioni 28, lakini hizi ni milioni moja

 =>Rais Magufuli: Kama mtu anaona ana haraka sana ya kuwahi anapokwenda, akapande ndege za jeshi awahi

 =>Rais Magufuli: Kutoka Dar hadi Mbeya, tofauti ya muda wa kufika kati ya ndege hii na Jet ni dakika 20 tu-

 => Rais Magufuli: Niwaombe watanzania tusipende kubeza, kama kitu hukitaki, basi ukae kimya

 =>Rais Magufuli: Tungenunua ndege hizi kwa kulipa polepole, tungekuja kulipa gharama kubwa, ndio maana tumelipa zote

 =>Rais Magufuli: Tuna mpango wa kununua ndege mbili kubwa, moja itabeba watu 160, nyingine itabeba watu 240

 =>Rais Magufuli: Tuliamua kununua ndege, tutazikodisha kwa ATCL, mwendo wa kucheza sasa umekwisha

 =>Rais Magufuli: ATCL ilikuwa haijiendeshi kibishara, walikuwa wapo tu, wanategemea serikali kila kitu

 =>Rais Magufuli: ATCL haikuwa ikijenga uchumi wa nchi na utalii kama ilivyokuwa inatakiwa

 =>Rais Magufuli: Maofisa wa ATCL walikuwa wakijilipa posho za TZS 50,000 kila wakitembelea uwanja wa ndege Dar es Salaam.

 =>Rais Magufuli: Vituo vya ATCL vya Comoro, Mwanza, Mtwara na Dar es Salaam, vilikithiri kwa ubadhirifu

 =>Rais Magufuli: ATCL walikuwa hawafuati ratiba, unaweza kuambiwa ndege inaondoka leo, lakini isiondoke hadi wiki moja

 =>Rais Magufuli: ATCL walikuwa wakijilipa overtime za uongo

 =>Rais Magufuli: ATCL walikuwa wakinunua mafuta hewa, unaambiwa ndege imeenda Mwanza kumbe iko Dar es Salaam uwanjani

 =>Rais Magufuli: Katika kituo cha Comoro, ilipotea TZS milioni 700, aliyepoteza akaongezewa muda ili apoteze nyingine

 =>Rais Magufuli: Bodi ya ATCL naomba mchambuwe wafanyakazi, chambueni kama Saida Karoli anavyosema, chambua kama karanga

 =>Rais Magufuli: Bodi ya ATCL msiogope kupunguza wafanyakazi, tulipunguza 500 wa NIDA, hawa hawatatushinda

 =>Rais Magufuli: Mfanyakazi kama unataka kuendelea kufanya kazi ATCL, utubu, uwe tayari kuwatumikia watanzania

 =>Rais Magufuli: Ndani ya ATCL kuna wake wa Mawaziri, Shirika halizalishi lakini wake wa Mawaziri wameng'ang'ani tu

 => Rais Magufuli: Wale ambao hawawezi kwenda na mwendo wetu, waje tuwalipe fedha zao watuache tufanyekazi

 =>Rais Magufuli: Haiwezekani wageni wakitaka kuja Tanzania, lazima watue nchi nyingine, hii ni aibu kubwa

 =>Rais Magufuli: Lakini mjue mnaenda kwenye ushindani, washindani wenu hawatawafurahia, mjipange vizuri kuwakabili-

 =>Rais Magufuli: Niwaombe Bodi ya ATCL, msitumie mawakala kukatisha tiketi zenu

 =>Rais Magufuli: Kuna wafanyakazi wa ATCL naona wapo wanafanya kazi tangu mimi nipo shule ya msingi

 =>Rais Magufuli: ATCL ya sasa ukiona hata sare za wafanyakazi zinatia kichefuchefu, hazitamaniki

 =>Rais Magufuli: Lakini niwaombe Watanzania tuwe wazalendo, tutumie usafiri wa ATCL ili tuweze kununua ndege nyingine

 =>Rais Magufuli: Niwaombe Bodi na Menejimenti, msimruhusu kiongozi asafiri bure, hata kama ni mimi, mnitoze nauli

 =>Rais Magufuli: Najua kunawakati ATCL mnajipendekeza kwa viongozi, lakini mjue mwishoni tutawapima kwa utendaji wenu

 =>Rais Magufuli: Hata kama ni kiongozi wa ATCL, ukisafiri hakikisha unalipa nauli, vitu vya bure ndivyo vinatumaliza-

 =>Rais Magufuli: Sasa tuna kazi ya kukarabati viwanja, shughuli hii tutaianza mapema sababu fedha tunazo

 =>Rais Magufuli: Sisi hatutaki kufukuza wafanyakazi, lakini watajifukuzisha wenyewe kutokana na utendaji wao

 =>Rais Magufuli: Ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar- Mwanza- Kigali- Bujumbura tayari tenda zimetangazwa

 =>Rais Magufuli: Tunataka kuanza ujenzi wa treni za umeme Dar es Salaam, haya si Ulaya tu, hata hapa yatafanyika

 =>Rais Magufuli: Ujenzi wa daraja la Coco Beach hadi Agha Khan umeanza, Interchange ya Ubungo itaanza karibuni

 =>Rais Magufuli: Mkoa wa Dar es Salaam, una jumla ya wanafunzi hewa 7000, Wafanyakazi hewa wapo 17,000

 =>Rais Magufuli: Hii nchi ilikuwa imefika pabaya, kila kona ukigeuka ni hewa, hewa, hewa

 =>Rais Magufuli: RAS, DED tuliowafukuza jana, leo wamefikishwa mahakamani, hii imesaidia Uingereza kutuchangia bilioni 6

 =>Rais Magufuli: Uingereza imetuchangia bilioni 6 sababu wameona wakitupa fedha zao zitafika kwa walengwa kule Kagera

 =>Rais Magufuli: Tunakagua vyeti ili kujua viwango vya elimu na sehemu watu waliposoma, lengo si kuwafukuza wafanyakazi

 =>Rais Magufuli: Ndugu zangu kazi hii ni ngumu, Mawaziri msiwaone, hawana raha hawa

 =>Rais Magufuli: Waandishi wa habari, ninyi ni muhimili kama ilivyo Bunge, tusaidiane tunapochukua hatua-

 =>Rais Magufuli: Waandishi wakati mwingine mnaandika habari za uongo kama nyie mna mahali pengine pakuishi ila si hapa

 =>Rais Magufuli: Watanzania mjue, tukishindwa sisi, tumeshindwa sote, tukiweza tumeweza wote

 => Rais Magufuli: No research, no right to speak, lakini hapa ni kinyume, watu hawajui lakini wanaongoza kuongea

 =>Rais Magufuli: Kama kungewezekana mtu ukiwa Rais baada ya miaka miwili na nusu unamuachia mwingine, mimi ningefurahi-

 =>Rais Magufuli: Natamani huyo aliyesema hazina spidi nimjue nimlipie nauli akae mbele aone zinavyokata mawingu-

 =>Rais Magufuli: Ninaishukuru CCM kwa kuandika ilani inayotekelezeka, naamini tutafanya zaidi

 =>Rais Magufuli: Mungu ibariki ATCL, Mungu bariki Bodi ya ATCL,


Mungu bariki wafanyakazi wazuri, Mungu ibariki Tanzania..........

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages