Breaking News

Your Ad Spot

Sep 17, 2016

IKULU YATAHADHARISHA UMMA KUHUSU BARUA FEKI INAYOSAMBAZWA KUOMBA FEDHA

GERSON MSIGWA
DAR ES SALAAM
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imewatahadharisha wananchi kuwa kuna watu wametumia nembo ya kurugenzi hiyo na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kuchapisha kisha kusambaza kwa barua kwa  kampuni binafsi na  Wakurugenzi Watendaji wa wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kinachodaiwa kuwa  rekebisho la Bajeti za miundombinu na mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge mjini Dodoma, Septemba 21, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Msigwa, imesema, barua hiyo kuhusu mkutano huo, haijaandikwa na Ofisi yake hivyo siyo ya kweli.

Ifuatayo ni Tarifa kamili kutoka Ikulu

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"

Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.

Yeyote aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.

Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Septemba, 2016

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages