.

DC SOPHIA MJEMA: JOGGING SIYO VICHAKA VYA WAHALIFU NA WAZEMBE

Sep 17, 2016

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema (wapili kulia) akiwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (watatu) wakishiriki mazoezi ya pamoja na kikundi cha klabu ya Mazoezi cha New Life Jogging,na vikundi vingine kadaa vya mazoezi, leo asubuhi katika viwanja vya Kimanga,Tabata Mawenzi,jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye mazoezi hayo ambayo yaliambatana na maadhimisho ya kikundi cha New Life Jogging kutimiza mwaka mmoja tangu kianzishwe
 Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, mwenye kofia nyeusi, akiendelea na mazoezi ya Jogging pamoja na vikundi mbalimbali 
 Vikundi mbalimbali vikiendelea na Jogging
 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikabidhiwa Risala na Mwenyekiti wa kikundi cha Newa Life Jogging,Baraka Urio akiwa ameambatana na wanachama wa kikundi hicho,mara baada ya kuisoma na kuelezea changamoto na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kikundi hicho.Kikundi hicho chenye makazi yake Tabata Mawenzi leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza ma vikundi mbalimbali vya mazoezi vilivyoshiriki kwenye hafla fupi ya kutimizwa mwaka mmoja  kikundi cha New Life Jogging. 

Mjema aliwataka wanaviikundi vya Joggingi, kutoishia tu katika mazoezi bali kutumia vikundi vyao katika kujijenga kiuchumi kwa kubaini fursa mbalimbali na kuzitumia.

Ametaka vikundi kuwa macho na kutoruhusu vikundi vyao kutumiwa na  wahuni na wahalifu mbalimbali wakiwemo watumia dawa za kulevya, panya rodi, makaka na madada poa.

Mjema amewataka viongozi wa vikundi hivyo kubaini changamoto na fursa wanazoona kuwa zinaweza kuwasaidia katika kuinua maisha ya wanavikundi wao na wanapobaini fursa au kukumbwa na changamoto wafike mara moja katika Ofisi yake ili kumuona mwenyewe au wasaidizi au maofisa katika ofisi yake.


"Lakini wale waliotaka kuingiza uhalifu,waliotaka kupenyeza madawa ya kulevya ,waliotaka kuingiza siasa,waliotaka kuingiza Panya rodi washindwe na walegee,hatutaki Jogging zetu zichafuke, tunataka Jogging zitumike kuona fursa zilizopo",alisema Mjema.
 Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo akiwasalimia na kuwatia moyo wanamazoezi wa vikundi hivyo vya Jogging,ambaye pia aliwaeleza kuwa wakati wa kujituna na kufanya kazi ni sasa,hivyo amewaomba viongozi wa vikundi hivyo kukutana nao ili kuhakikisha fursa na changamoto walizozieleza katika risala yao zinafanyiwa kazi kwa wakati.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa kikundi cha New Life Jogging,Baraka Urio,pichani kati ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo na wadau wengine wakishuhudia tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na viongozi wengine waandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha New Life Jogging,ambacho leo kinasherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª