Dk Ali Akbar Salehi, Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Ira
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran
amesema kuwa ujenzi wa vinu viwli vipya vya nishati ya nyuklia utaanza
katika mji wa Bushehr kusini mwa Iran tarehe kumi mwezi huu wa Septemba.
Ali Akbar Salehi amesema kuwa,
mapipa milioni 22 ya mafuta yataokolewa kila mwaka hapa Iran baada ya
kujengwa vinu hivyo vya nyuklia.
Salehi amebainisha kuwa ujenzi wa vinu
hivyo viwili vya nyuklia unatabiriwa kuchukua muda wa miaka kumi na
kwamba mradi huo utagharimu dola bilioni kumi za Kimarekani.
Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya
Iran pia amesema, Tehran itashirikiana na Russia kwenye ujenzi huo na
kueleza kuwa mkataba huo umefikiwa kwa kuzingatia kushirikishwa
vilivyo kiufundi viwanda vya ndani ya Iran katika utekelezaji wa mradi
huo.
Ali Akbar Salehi ameashiria uwezo wa
Iran katika sekta ya nishati ya nyuklia na kubainisha kuwa, Tehran
itakuwa na nafasi muhimu sana katika sekta ya nyuklia kwenye kipindi cha
miaka kumi ijayo kwa kuzingatia mahitaji ya nchi katika kulinda na
kudhamini maslahi ya wananchi hususan katika nyanja za nishati, viwanda,
kilimo na tiba.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269