Kamanda wa mkoa wa Njombe wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkaguzi Joseph
Mwasabeja akitoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwa wanafunzi
wa shule ya Sekondari Njombe
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakifanya ukaguzi wa mifumo ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto katika moja ya majengo marefu hapa jijini
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi ya uzimaji moto
na kiasi cha maji yanayotumika (Pressure) wakati wa matukio
LIJUE
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA MAJUKUMU YAKE KATIKA KUTEKELEZA DHIMA YA KUOKOA
MAISHA NA MALI ILI KUKUZA USALAMA KWA UMMA, KUPOKEA MIITO YOTE YA DHARURA,
KUTOA MSAADA NDANI YA JAMII KWA UFANISI NA KWA MUJIBU WA MWONGOZO WA SERA YA
TAIFA NA VIWANGO VYA KIMATAIFA.
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE
AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga
yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na
majanga mengineyo.
HUDUMA
YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI INATOLEWA.
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji limeundwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. Hivyo basi
mtu yeyote anastahili kupata huduma hiyo kwa kupiga namba ya simu 114. Pia kuna
huduma nyingine zitolewazo na Idara.
HUDUMA
ZITOLEWAZO NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji linajukumu kubwa la kutoa huduma kwa jamii katika Nyanja mbalimbali
zikiwemo Kuokoa maisha ya watu na mali zao, Kuzima moto, Kutoa elimu ya kinga
na tahadhari ya majanga moto, Kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto, Kusoma ramani za majengo na kutoa
ushauri, Kutoa huduma ya kwanza katika majanga na ajali barabarani, Kutoa
mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto, Kufanya uchunguzi kwenye majanga ya
moto na Kutoa huduma za kibinadamu.
KUFIKA KWENYE TUKIO
BILA YA VITENDEA KAZI (MAJI)
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wote huwa limejiandaa kwa magari yake
kuwa na vitendea kazi vya kuzimia moto na kufanyia maokozi pia magari huwa
yamejazwa maji wakati wote yanapokuwa vituoni yakisubiri matukio. Changamoto
iliyopo ni wananchi wengi kuwa na dhana kuwa magari ya Zimamoto huenda kwenye
matukio bila maji.
AINA YA GARI LA
ZIMAMOTO, VIFAA, UWEZO WA KUBEBA MAJI (UJAZO), NA JINSI YA UFANYAJI KAZI
Gari la Zimamoto linapofika kwenye tukio hufanya kazi kama mtambo wa
kuzimamoto, magari hayo yanamatanki ya maji yenye ujazo kuanzia lita 1,500 hadi
lita 7,000 (kuna moja linabeba lita 16,000) ili maji hayo yatoke kwa nguvu na
kuweza kuzimamoto, magari ya Zimamoto yamefungwa pampu zenye uwezo wakusukuma
lita 2,000 hadi lita 6,000 kwa dakika.
Kwa kawaida tunapofika kwenye tukio hutumia mipira yenye kipenyo cha
milimeta 70 na kufunga kifaa cha
kumwagia maji (branch pipe) chenye kipenyo cha milimeta 20 na pampu husukuma
maji kwa nguvu ya bar 7, kwa vipimo
hivyo huwa tunamwaga lita 1,000 kwa dakika kwa njia moja ya kutolea maji hivyo
kwa gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha ndani ya dakika saba, kwa
kawaida tunatumia njia mbili za kutolea maji hivyo huwa tunamwaga lita 2,000
kwa dakika, na gari lililobeba lita 7,000 maji yatakwisha baada ya dakika 3½
nasisi hulazimika kuondoka eneo la tukio kwenda kutafuta maji.
Huku nyuma wanaweza kuja waandishi wa habari na kuwauliza wananchi mbona
moto unawakana Zimamoto hawapo? Wananchi hujibu kuwa wamekuja lakini baada ya
muda mfupi wameondoka na kusema kuwa wanakwenda kuchukua maji, hapo ndipo dhana ya Zimamoto wamekuja kuangalia kwanza ukubwa wa moto na sasa ndio wamekwenda
kuchukua maji hujengeka. Ki uhalisia si kweli kuwa magari ya Zimamoto hufika
kwenye tukio bila ya maji.
Maji yanayobebwa na magari ya Zimamoto husaidia kuanzia kazi, kabla maji
ya kwenye gari kwisha gari la Zimamoto hutegemea kupata maji kutoka kwenye
vituo maalum vya maji kwa ajili ya Zimamoto (Fire Hydrants) ambazo katika miji
yetu mingi huwa hazifanyi kazi kutokana na sababu zifuatazo:-
(i)
Kutokuwa na
maji
(ii)
Kufukiwa na
vifusi au mchanga au kufunikwa kutokana na ukarabati wa mitaa au barabara.
(iii)
Kung’olewa na
kubadilishwa matumizi.
(iv)
Kung’olewa kwa
alama za utambulisho (H sign)
(v)
Kuibiwa kwa
mifuniko kutokana na biashara ya chuma cha kavu.
(vi)
Miradi mingi
ya maji katika miji kutoshirikisha ufungwaji wa vituo vya maji (Fire Hydrants).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269