Jumamosi
Septemba 10, 2016 kuamkia leo jumapili, kinyang'anyiro kikali cha
kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016),
kimefanyika ambapo Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka
mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa walimbwende 17 (baada ya
mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.
Ushindi
wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria
kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall
Jijini Mwanza, likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions
chini ya Mkurugenzi wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni
mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na
102.5 Lake Fm Mwanza.
Mbunge
wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema
ni furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016
na kwamba matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la
Miss Tanzania 2016 ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza
mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016.
Na BMG
Mlimbwende,
Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi wa
Ozona Miss Lake Zone 2016, miongoni mwa walimbwende 17 waliokuwa
wakiwania taji hilo.
Mlimbwende
wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka
mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto)
na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Mlimbwende
wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (katikati) kutoka
mkoani Geita. Mshindi wa pili ni Mery Peter (Miss Mwanza 2016, kushoto)
na Mshindi wa tatu ni Lucy Michael (Geita, kulia).
Aliyekuwa akishikilia taji la Miss Lake Zone
Aliyekuwa Miss Lake Zone (kulia), akikabidhi taji la Miss Lake Zone mpya (kushoto)
Mgeni
rasmi, Mkuu wa Wilaa ya Nyamagana, Mhe.Mary Tesha (kushoto) akimkabidhi
mshindi wa Ozona Miss Lake Zone mfano wa ufunguo wa gari alilokabidhiwa
kama zawadi. Mshindi wa Ozona Miss Lake Zone amewazadiwa gari lenye
thamani ya shilingi Milioni 12 na kampuni ya Ozona.
Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, Mshindi wa Ozona
Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick, Mbunge wa Jimbo la Geita
Vijijini, Joseph Msukuma pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ozona,
Dr.Thobias Mkina, wakiwa katika picha ya pamoja.
Mshindi
wa Ozona Miss Lake Zone 2016, Eluminatha Dominick (kushoto) akiwa
katika picha na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma
(kulia).
Washiriki
walioingia nafasi tano bora ni, Eluminatha Dominick (wa pili kushoto
kutoka Geita), Mery Peter (wa tatu kushoto kutoka Mwanza, Lucy Michael
(wa kwanza kushoto kutoka Geita), Rose Masanja (wa pili kushoto kutoka
Shinyanga) na Farida Hassan (wa kwanza kulia kutoka Mara).
Washiriki 17 wa Ozona Miss Lake Zone 2016
Ozona Miss Lake Zone akizungumza na Wanahabari baada ya kukabidhiwa gari
Mchekeshaji Eric Omond kutoka nchini Kenya akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya show
Kushoto ni Christian Bella, akizungumza na Vesterjtz wa BMG baada ya kudondoka burudani kali
Katikati ni mbunge Joseph Msukuma akizungumza na BMG
Kulia ni mmoja wa wanakamati akihojiwa na BMG
George Binagi-GB Pazzo (ushoto) katika picha ya pamoja na Christian Bella (kulia) baada ya show
Mwanahabari Sadam Sadick (kulia) akishow love na Bella
Ozona Miss Lake Zone 2016 (kushoto) akiwa na Vesterjtz
Kijukuu kutoka RFA akiwa na Ozona Miss Lake Zone 2016
Mambo ya karanga fotooo na Ozona Miss Lake Zone 2016
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269