Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba,
Kanisa Katoliki, Methodius Kilaini, akibariki leo Septemba 11, 2016,
majeneza 16 yaliyobeba miili ya watu waliofariki kutokana na madhara ya
tetemeko la ardhi lililokumba mji wa Bukoba mkoani Kagera Septemba 10,
2016. Watu 16 wameripotiwa kupoteza maisha hadi hivi sasa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Kanisa Katoliki, Methodius Kilaini, akiongoza ibada hiyo
Waziri Mkuu kassim Majaliwa akiwasili
kwenye uwanja wa michezo wa Kaitaba alasiri hii Septemba 11, 2016
kuongoza ibada ya kuaga miili ya watu 16 waliofariki kwenye tetemeko
hilo
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Kanisa Katoliki, Methodius Kilaini, akiongoza ibada hiyo
Majeneza ya watu waliouawa kwenye
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016, yakiwa
yamepangwa kwenye uwanja wa michezo wa Kaitaba mjini Bukoba leo Septemba
11, 2016 tayari kwa i bada ya kuwaaga itakayoongozwa na waziri mkuu
Kassim Majaliwa muda mfupi ujao. Watu 16 wameripotiwa kufariki dunia
hadi leo hii kutokana na tetemeko hilo lililokumba maeneo yanayozunguka
ziwa Victoria ambapo Manispaa ya Bukoba ndiyo iliyoathirika zaidi.
Wataalamu wa jiolojia wa Marekani
wanasema tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha Richa 5.7 na
lililokwenda umbali wa kilomita 10 chini ya ardhi, limezikumba nchi za
Uganda na Rwanda. Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo, amesema
watu 200 wanapatiwa matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya Bukoba.
Waombolezaji wakiwa kwenye uwanja wa Kaitaba tayari kwa ibada hiyo
Waombolezaji wakiwa kwenye uwanja wa Kaitaba tayari kwa ibada hiyo
Waombolezaji wakiwa kwenye uwanja wa Kaitaba tayari kwa ibada hiyo
Baadhi ya majeruhi wakisubiri kupatiwa huduma kwenye hpspitali ya rufaa ya Bukoba Septembe 10, 2016.
Hii ni moja kati ya nyumba kadhaa zilizobomolewa kutokana na kishindo cha tetemeko hilo. (PICHA NA FAUSTINE RUTA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269