Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA), aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege
akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama
hicho baada ya kufanyika uchaguzi wilayani humo jana.
Mwenyekiti mpya Jesse John, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa chama hicho na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.
Na Dotto Mwaibale, Kisarawe
MTANGAZAJI nguli wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA) katika uchaguzi
uliofanyika jana.
Jesse ambaye aliupata uongozi huo katika
uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa aliibuka kidedea baada ya kupata
kura 32 na kumshinda mpinzani wake Karim Wenge aliyepata kura 21.
Katika uchaguzi huo Mohamed Lubondo
alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata kura 30 na kumshinda Francis
Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi alichaguliwa kuwa Amosi
Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa Abdul Mogella.
Wasimamizi wa uchaguzi huo kutoka Chama
Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Mweka Hazina wa KIDIFA
alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa kuwa
Sadiki Nasoro.
Mwakilishi wa klabu kutoka Tarafa ya
Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge, kutoka Tarafa ya Sungwi
alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa klabu alichaguliwa kuwa Ally
Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed
Masenga.
Mwenyekiti wa KIDIFA aliyemaliza muda
wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse kushukuru wajumbe aliwataka
viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji vya vijana katika soka wilaya
ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano mbalimbali yenye lengo la kutafuta
vipaji.
Jesse akiwashukuru wajumbe hao aliahidi
kushirikiana na wadau wa soka ndani na nje ya wilaya hiyo kupata timu ya
wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kama timu nyingine
zinashiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti Jesse alisema wilaya ya
Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili alisema anaamini vijana wengi
hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hivyo atatumia miaka minne ya
uongozi kuzalisha vijana wazuri katika soka.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269