.

MUWSA YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MANDELA MJINI MOSHI.

Sep 7, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Saidi Meck Sadiki akiwasili katika shule ya msingi Mandela iliyopo kata ya Bomabuzi wilaya ya Moshi kwa ajili ya kupokea msaada wa Madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiimba nyimbo wakati wakipokea wageni waliofika katika tukio la kukabidhi madawati.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki alipowasili katika shule ya msingi Mandela kwa ajili ya kukabidhiwa Madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki akiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya (kulia) wakati wa makabidhiano ya Madawati kwa ajili ya shule ya msingi Mandela.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) ,Joyce Msiru akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati kwa ajili ya shule ya msing Mandela.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro , Saidi Meck Sadiki Madawati kwa ajili ya shule ya Msingi Mandela iliyopo Manispaa ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro , Saidi Meck Sadiki (katikati) akiwa ameketi kwenye Dawati na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru pamoja na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela.
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mandea wakiwa wameketi katika madawti yaliyotolewa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki akikabidhi madawati kwa mkuu wa shule ya msingi Mandela ,Pegi Michael.

Na Dixo Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช