Breaking News

Your Ad Spot

Sep 20, 2016

POLISI MAREKANI YAMKAMATA MSHUKIWA WA SHAMBULIO

Shambulio la Bomu Marekani
Shambulio la bomu Marekani
Mtu aliyekuwa akitafutwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu katika miji ya New York na New Jersey amekamatwa baada ya kushambuliana na polisi kwa risasi.
Ahmed Khan Rahami, mwenye umri wa miaka 28 ni raia wa Marekani mwenye asili ya Afghan.

Alijeruhiwa katika mapambano hayo yaliyosababishwa kukamatwa kwake karibu na nyumba yake kwenye mji wa New Jersey.

Katika operesheni ya kumkamata mtuhumiwa huyo polisi wawili pia walijeruhiwa.

Meya wa mji wa New York, Bill de Blasio amesema kuna kila sababu kuamini kwamba shambulio hilo lilikuwa ni ugaidi.
Kwa upande wake Rais Barack Obama amewataka watu kuwa watulivu na kuongeza kuwa kila mtu ana mchango katika kuondoa hali hiyo. BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages