Breaking News

Your Ad Spot

Sep 20, 2016

17 WAPOTEZA MAISHA WAKATI WA MAANDAMANO YA UPINZANI

media
Katika mtaa wa Limete, mjini Kinshasa, mamia ya watu walikusanyika katika eneo linalojulikana kwa jina la Lumumba, DRC, Jumatatu Septemba 19, 2016.

Wizara ya mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba watu 17 ndio wamepoteza maisha katika maandamano ya upinzani wakidai kuondoka madarakani kwa rais Joseph Kabila atakapomaliza muhula wake mwezi Desemba mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa DR Congo, Evariste Boshab aamesema watu 17 wamepoteza maisha katika maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na askari polisi watatu.

Watu hawa wamepoteza maisha wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumatatu hii katika mji wa Kinshasa na miji mingine ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congoongo, Lambert Mende, askari polisi walichomwa moto wakiwa hai na raia waliouwawa walikuwa miongoni mwa waandamanaji.

Watu kadhaa wamekamatwa. Miongoni mwao ni wabunge wawili wa upinzani, ikiwa ni pamoja na Martin Fayulu.

Upinzani nchini DR Congo ulifanya maandamano katika miji kadhaa nchini kote Jumatatu hii, wakidai uchaguzi wa urais ufanyike mwezi Novemba, kama inavyotakiwa na Katiba.
Lakini uchaguzi wa urais hauwezi kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka, kulingana na viongozi wa vyama vinavyounga mkono serikali na viongozi wa Tume ya uchaguzi ya Taifa. RFI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages