Breaking News

Your Ad Spot

Oct 16, 2016

KIONGOZI WA UPINZANI KIZZA BESIGYE AKAMATWA NA POLISI

media
Kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye akisindikizwa na maofisa wa gereza la Luzira alikokuwa akishikiliwa
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Daktari Kizza Besigye amekamatwa na polisi jumamosi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kasangati wilayani Wakiso.

Muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake Dr Besigye,kama kawaida alirushiana maneno na mkuu wa polisi wa kituo cha Kasangati Bwana Robert Kachumu.

Daktari kizza Besigye alikamatwa baada ya kutomjibu afisa huyo wa polisi ambaye alitaka kujua Kizza Besigye anaenda wapi.

Kwa mujibu wa Daily Monitor la nchini Uganda Kizza Besigye alijitetea kuwa ana haki ya kutembea kama raia wengine.
Besigye analaani kuzuiwa nyumbani na uwepo wa askari wengi kuzunguka makazi yake.

Besigye ambaye alikuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha FDC alikamatwa masaa kadhaa baada ya kundi la wanachama wa upinzani kuwaambia waandishi wa habari kuwa wana mpango wa kuligawa bunge kufuatia kuzuiwa nyumbani kwa kiongozi huyo.

Inaelezwa kuwa Daktari Kizza Besigye anashikiliwa katika kituo cha polisi Nagalama wilayani Mukono.RFI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages