Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani,
Stellah Mtayabarwa (kushoto), akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), alipotembelea banda
la Saccos la Mamlaka ya Bandari (PTA), katika ufunguzi wa maadhimisho
hayo uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard
Kalinga (katikati), akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo, Stellah Mtayabarwa.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho hilo, Habibu Mhezi (kulia), akizungumza kwenye
mkutano huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar
es Salaam, Mrakibu wa Polisi (SP), Scholastica Luhamba.
Mjasiriamali
Zamda Sasillo (kushoto), akiwa na wateja walitembelea banda lake katika
maadhimisho hayo. Kutoka kulia ni Magdalena Samkumbi, Lubanzo Kalufya
na Ashura Shoka.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na Ofisa Uendeshaji Mkuu, Mfuko wa Pembejeo, Pili Mogasa.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Ofisa
Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Ezekiel Fumbo (kushoto),
akimuelekeza Dk. Turuka kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Viongozi Meza kuu wakipiga makofi wakati wakipokea maandamano ya maadhimisho hayo.
Wadau wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Wasanii
wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikionesha umahiri wa
kucheza ngoma aina ya chaso inayochezwa na wenyeji kutoka Pemba.
Hapa ni mserebuko wa ngoma ya chaso ya wenyeji wa Pemba.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na vyama vya akiba na mikopo ili kujenga mazingira bora ya kuinua uchumi nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk.
Florens Turuka wakati wa ufunguzi wa Siku ya Saccos duniani uliofanyika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
"Vyama
vya akiba na mikopo ni wadau wakubwa wa serikali kwani vinasaidia sana
katika kiinua uchumi wa nchi hivyo hatuna budi kuendelea kushirikiana"
alisema Dk.Turuka.
Dk.
Turuka aliwataka viongozi wa vyama hivyo kumaliza changamoto zao wao
wenyewe na wanachama wao pale zinapotokea badala ya kukimbilia
serikalini.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard
Kalinga alisema vyama hivyo vimepata mafanikio makubwa kwani
wamefanikiwa kuanzisha Saccos 4,000 ambazo zipo hadi vijijini na kuwa na
wanachama milioni 1.5 nchini.
"Sheria
namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 imeanza kutumika baada
ya kupata idhini ya Rais mwezi Oktoba 2013 lakini ni dhahiri kuwa
kumekuwa na malalamiko mengi juu ya baadhi ya maeneo yaliyoko kwenye
sheria hiyo" alisema Kalinga.
Alisema
licha ya kupata mafanikio hayo changamoto kubwa waliyonayo ni
ushirikishwaji wa kuandaa sheria inayoongoza vyama vya ushirika nchini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269