.

WAFANYAKAZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH) WAMEAHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA PROFESA MUSERU

Oct 11, 2016

Mkuu wa Idara ya Tiba wa hospitali hiyo, Dk. Olivia Rusizoka akitoa neno la ukaribisho kwa waalikwa baada ya kufungua kwa Sala maalum katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dr, Hedwiga Swai  akifungua rasmi hafla hiyo wa kuwaaga wafanyakazi 4 waliostaafu kwa mujibu wa Sheria 
Waalikwa
Baadhi ya wakuu wa idara na waalikwa

Baadhi wa waalikwa ambani wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili


Wafanyakazi wakionyesha umahiri wao kwa kucheza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu 4 waliomaliza muda wao kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili (MNH) Profesa Lawrence Museru
Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira ya Ndani Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Zuhura Mawona (kushoto) akiomba Dua wakati wa kupata chakula cha jioni kilicho andaliwa na kulia ni Mkuu wa Idara ya Tiba wa hospitali hiyo, Dk. Olivia Rusizoka


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru (kushoto) akikabidhiwa zawadi na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupongezwa kwa kuthibitishwa kwake na Rais John Pombe Makufuli  wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi 4 waliostaafu kwa mujibu wa sheria

 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameahidi kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru baada ya kudhibitishwa na Rais Dk. John Magufuli.
 
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Daktari Bingwa wa Kisukari wa hospitali hiyo, Dk. Wolfgang Bernard katika hafla ya Wakuu wa idara ya Tiba wakati wa kuwaaga wafanyakazi wa MNH wanne waliostaafu kwa mujibu wa Sheria.
 
Alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kumthibitisha Prof. Museru na kumuombea dua,  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na viongozi wote walioshiriki kufanya uamuzi huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Tiba wa hospitali hiyo, Dk. Olivia Rusizoka kwa niaba ya   wafanyakazi wote alimshuru Rais Magufuli kwa kumthibitisha Profesa  Museru .

Rusizoka alisema kuwa wamejipanga kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mkurugenzi huyo ili kufanikisha shughuli za kiutendaji hospitalini hapo.


"Sisi wafanyakazi wote tunamshukuru sana Rais wetu kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga nchi yetu, kikubwa kwetu ni kumuombea Dua kwa Mungu ili awe na maisha marefu yeye na wasaidizi wake wawe na afya njema wao na familia zao pia tutatoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkurugenzi aliyemteua," alisema.

Museru kabla ya kuteuliwa kwake kuiongoza Hospitali ya Taifa Muhimbili alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI na kustaafu na ndipo Rais akamteua kukaimu nafasi hiyo na hivi karibuni alimthibitisha.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช