Mkurugenzi
wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari
Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa
Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.
Na George Binagi-GB Pazzo
"Hii
mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki
kwa sasa, kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji
wa viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni
Kibamba.
Ameshikilia
msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini
Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini
kwake.
Leo
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia
msimamo wao wa kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na
Watendaji Jijini Mwanza.
Juzi
jumamosi Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja
kikao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka
kukabidhi mihuri yao.
BMG ,Mwanza
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269