Afisa
Mtendaji Athumani Mtono (kushoto) akisoma Taarifa za Kata mara baada ya
kuwasili Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ( wa pili kulia) katika
ziara aliyoifanya katika Kata ya Tandale Jijini Dar es Salaam, wa
kwanza ni Diwani wa Kata hiyo na ni Naibu Meya wa Kata hiyo, Jumanee
Amir Mbunju
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
STORY YA ZIARA YA MKUU wa WILAYA HAPPY
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happy amewataka Watendaji wote katika Wilaya hiyo kuacha kukaa ofisini na kwenda mtaani kusikiliza kero za wananchi ili Serikali iweze kuzitatua shida za wanchi wake.
Aidha amewataka kutembelea Nyumba za wageni zote ili kujua kama wana leseni halali ya biashara na siyo vivuli vya leseni hizo huku akiwaagiza kuhakikisha hakuna bar wa kilabu kinachofunguliwa muda wa kazi.
Kauli hiyo ameitoa Dar es Salaam jana wakati wa ziara yake katika Kata ya Tandale ili kupokea taarifa mbalimbali na kero kutoka kwa viongozi na wananchi wa Kata hiyo.
Pamoja na kusikiliza kero toka kwa wananchi pia alifanya vikao na Watendaji na wataalam wa Kata hiyo na Kamati ya maendeleo ya Kata.
Mkuu huyo aliwataka viongozi kuweka agenda ya Ulinzi na usalama kuwa ya kwanza kwenye vikao vyao ili wananchi waweza kufanya kazi kwa amani na usalama.
Pia aliwataka Watendaji wote na wataalam kuwa na Mipango mikakati na kuwasikikiza wananchi matatizo yao kwa kuwa wameajiliwa kwa ajili yao.
Alisema lengo kubwa la ziara yake ni kuwasikikiza wananchi kwa kuwa ameletwa Wilayani hapo kiwatumikia na hayuko tayari kukaa ofisini wakati wananchi hawawezi kufika wote ofisini na hivyo kuwataka viongozi hao kuiga Mfano kwake.
Aliongeza kuwa mwisho wa ziara afisa utumishi atakuwa na taarifa za watumishi ambao hawaendani na kasi ya Serikali ya awamu ya tano na hawatawavumilia.
"Kuna Watendaji jeuri na viburi hawataki kusikiliza wananchi badala yake wanawanyanyasa ukibainika ama zangu ama zako" alisema.
ULINZI NA USALAMA.
Alisema hataki kusikia yaliyotokea Buguruni ya mtu kunyang'anya watu, kuwatoa macho na kuendelea kutesa mtaani huku akitamba mtaani.
"Sitaki kusikia katika Wilaya yangu yale yaliyotokea Buguruni, mtu kufanya uhalifu alafu anatamba mtaani, OCD nyie mnajua cha kuwafanya imarisheni vikosi vya ulinzi shirikishi na kila mmoja ajue jirani yake ni nani na anafanya kazi gani " alisema Happy
Happy aliwataka wenyeviti wote kuhakikisha wapangaji wote wanafahamika na kila anayehamia katika Wilaya hiyo kuwa na barua ya alikotoka na ithibitishwe na mjumbe.
Katika ziara hiyo Happy alikagua mradi mbalimbali kama shule za msingi, soko, kituo cha maji, Kituo cha watoto yatima cha Al Madina, kikundi cha mama lishe ili kujionea ubavu wa miundombinu na kupokea kero zao.
Baada ya kumaliza kukagua mradi hiyo alifanya mkutano wa Hadhara na wananchi wa Kata ya Tandale ili kutoa majibu ya jumla kutokana na kero alizopokea wakati wa ziara yake.
Mkuu wa Wilaya huyo anategemea kuzunguka Kata zote 20 za Wilaya hiyo ili kuendelea kujua kero na changamoto zinazowakabili.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269