.

WAZIRI UMMY ATEMA CHECHE KWA WAUGUZI-KIGOMA

Oct 6, 2016
Na Magreth Magosso,Kigoma

WAZIRI wa Afya Maendeleo Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amelitaka Baraza la wauguzi na Ukunga Nchini wasisite kufungia vyeti vya wauguzi na wakunga pindi wanapofanya kazi bila kuzingatia maadili na weledi katika  huduma watoazo kwa wananchi.


 

Pia amesema sekta ya afya imevamiwa na wauguzi feki na wataalamu feki hali inayoidhofisha taaluma hiyo kwa wananchi kutokana na watu wachache wanaotumia vyeti feki kufanikisha mambo yao na kuahidi kuwafukuza kazi wakati wowote, pindi watakapokamilisha mchakato wa utoaji wa ajira lakini kwa sasa wizara inashindwa kuwafukuza kutokana na mchakato wa ajira hiyo.

 

Akitoa kauli hiyo jana kigoma Ujiji Mkoa wa Kigoma kwenye Mkutano mkuu wa wauguzi ulilenga kuzungumzia utendaji kazi wa kada hiyo ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  vifaa na vifaa tiba ilihali wanafanya kazi kwa 80% zaidi ya Daktari huku wakikabiliwa na mishahara duni.

 

Waziri huyo alisema pamoja na changamoto zinazowakabili isiwe kigezo cha kutoa huduma mbovu kwa wagonjwa bali wazingatie madili na weledi wa huduma zao kwa mujibu wa waraka wa uuguzi,ili kupunguza maradhi mbalimbali yanayowakabili ananchi .

 

Alisema sekta ya afya inavamiwa na wataalamu feki kila kukicha na wapunguze skendo katika vyombo vya habari vya kutoa huduma mbovu kwa wananchi na wandishi watoe habari kwa muguzi aliyekosea si wauguzi wa kituo cha afya lalamikiwa sambamba na wananchi wasiwatishie wauguzi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

 

Alisema waganga wakuu wa mikoa na wafawidhi waweke utaratibu mwepesi wa wananchi kutoa malalamiko yao kwa wauguzi wasiotenda haki kwa wagonjwa ili sheria za nidhamu zichukuliwe kwa walengwa kabla ya kufika ngazi ya juu ili kudumisha umoja na mshikamano baina ya wagonjwa na wahudumu hao.

 

Mbali na hilo amewahakikishia watapewa nafasi ( scholarship )maalumu kwa wauguzi kwenda kuongeza ujuzi wa kutoa matibabu  hasa taaluma za ubingwa wa magonjwa mbalimbali na kuhusu suala la posho wakurugenzi na waganga wakuu wawajibike katika kutoa sare za wauguzi.

 

“wakurugenzi wa hospitali za umma,halmashauri  toeni posho za sare z ash.300,000 kila mwaka wapewe kabla ya siku 60,tutaoa barua kwa wakurugenzi watoe fedha hizo,wasipolipa fedha hizo kwa wauguzi watawajibishwa ,siwezi kuliachia hilo tutapelekana pabaya”alifafanua Mwalimu .

 

Hivi msipowapa sare za kazi wavae madila na pensi,mbona madawati mliweza kuchongesha ,Mimi sio mpuuzi na mtoe kadi za bima ya afya kwa wazee ,wauguzi wanatoa hduma zaidi ya daktari wanatumia muda mwingi kumuhudumia mgonjwa “alisema Waziri  huyo.

 

Awali  Raisi wa Chama cha wauguzi  Tanzania National Nurse Association(TANNA) Paulo Magesa alisema serikali iboreshe mifumo katika sekta ya afya kwa kuwa rasilimali watu yan taifa inabebwa na utendaji kazi wa wauguzi kwa 80% sambamba na kuitaka serikali iwape kipaumbele katika sehemu za mamuzi ya serikali na kumuomba awe sauti ya wauguzi ili kutatua changamoto zinazowakabili.

 

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha TANNA Taifa  Mark Ogweyo alisema viongozi wa serikali wanatumia vibaya madaraka yao pindi wanapopata tuhuma dhidi ya wauguzi wanaotuhumkiwa na jamii husika kwa kuwasimmisha kazi bila kufanya upelelezi wa kutosha hali inayowapunguza morari ya utendaji kazi kwa jamii husika.wakati kauli mbiu ya mkutano huo ni Nguvu ya Mbadiliko katika Mfumo wa Afya.

Mwisho.


--


Magreth Magosso
Jamboleo news paper
0757736863

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช