Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
amekanusha madai kuwa serikali yake inazipuuza nchi jirani na kujikita
zaidi katika masuala ya ndani.
Akizungumza
Jumatatu akiwa katika safari yake ya kwanza nchini Kenya tangu aingie
madarakani Novemba mwaka jana , Dkt. Magufuli amesema daima amekuwa
akiwasiliana na Rais Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu. Ameongeza kuwa
Tanzania inaitambua Kenya kama 'mshirika wetu nambari moja wa kibiashara
barani Afrika.' Amesema safari yake nchini Kenya inalenga kuimarisha
zaidi uhusiano wa nchi mbili ambao umekuwa mzuri tokea siku za nyuma.
Magufuli amesema amemfahamisha Rais Kenyatta kuhusu uhalisia wa mambo
nchini Tanzania ambao ni kuwashurutisha Watanzanai walipe kodi na
kupambana na ufisaid ili nchi isonge mbele.
Rais
Magufuli amekaribishwa kwa taadhima na heshima kubwa iliyojumuisha
kukagua gwaride kamili la jeshi iliyoandamana na mizinga 21. Punde baada
ya kuwasili, Rais Maguduli aliweka shada la maua katika kaburi la
mwanzilishi wa taifa la Kenya, Mzee Jomo Kenyatta kabla ya kuelekea
Ikulu ya Rais kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wake.
Viongozi hao wamejadili masuala ya uhusiano wa nchi mbili na kieneo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269