Timu ya
Chelsea imepata ushindi wake wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji
Southampton Mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mechi iliyochezwa katika
uwanja wa Mtakatifu wa St.Marry’s.
Wageni
walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Eden Hazard dakika ya sita
baada ya kuwachambua mabeki wa Southampton na mfungajia akipiga mpira wa
chini chini na kumuacha mlinda mlango Forster akiwa hana la kufanya.
Baada ya
kufungwa bao hilo Wenyeji walicharuka na kuliandama lango la Chelsea
kama nyuki kutokana na mfumo wa Conte wakutumia wachezaji watano
katikati huku nyuma akiweka watatu na kumubakiza mtu mmoja mbele
uliwambana vilivyo wenyeji na kushindwa kupenya ngome ya wageni hadi
mapumziko Chelsea walikuwa mbele ya bao moja.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Chelsea kupata bao dakika ya 55 kupitia kwa, Diego
Costa baada ya kupokea pasi safi toka kwa kiungo mkabaji Matic huku
likiwa bao lake la 7 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji kwenye msimamo
wa Ligi hiyo.
Kwa
matokeo hayo Chelsea wamepanda hadi nafasi ya nne ya msimamo wakiwa na
alama 22 kwa michezo yao kumi wakati Southampton wamebaki nafasi ya tisa
na alama 13.
VIKOSI:
SOUTHAMPTON
(4-3-3-):Forster; Martina, Fonte, Van Dijk, Bertrand (McQueen 78);
Romeu, Clasie (Boufal 61), Davis; Redmond, Tadic (Hojbjerg 78), Austin
SUBS NOT USED: Yoshida, Ward-Prowse, Taylor, Olomola
CHELSEA
(3-4-3):Courtois; Azpilicueta, Luiz, Cahill; Moses (Ivanovic 87), Kante
Matic, Alonso; Pedro (Willian 78), Costa (Batshuayi 89), Hazard
SUBS NOT USED: Begovic, Oscar, Terry, Chalobah
GOALS: Hazard 6, Costa 55
REFEREE: Mike Jones
ATTENDANCE: 31,827 (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269