Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme
ncini Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana
hati za mkataba na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa
kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya
kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line)
itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es
Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na kampuni tatu
kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na
Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo
la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
309.26
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na kampuni tatu
kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha
Tanzania na Kenya.
Hafla
ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya TANESCO
jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali,
limetiliana saini mikataba hiyo na kampuni ya Bouygues Energies Service,
Energoinvest na Kalpa-Taru.
Akizungumz
wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi
Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia
Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kisha
Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita
96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania
na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa Msongo wa
Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
“
Napenda niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa
na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande
zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.
Akifafanua
zaidi, Mhandisi Mramba alisema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki
ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan,
(JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika
kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
“Dola
za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika
kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo kwa wakandarasi waliopewa kazi hiyo
kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“
Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo
tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa
mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO hatutakubaliana na hilo.”
Alionya Mhandisi Mramba.
Naye
mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo
itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la
Afrika.
Kwa
upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na
AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA,
katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service,
Patrick Canton wakisaini mkataba huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba
Mhandisi Mramba, (kushoto), na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakisaini
mkataba kutekeleza mradi huo
Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, akizungumza
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati
wa hafla hiyo. Kulia ni Bi. Rosina wa JICA
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
Mratibu wa Miradi wa Shirika la Umeme
nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), akizungumza
wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na Mwakilishi mkazi wa
AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha ya pamoja na
wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa mradi huo
Kutoka kushoto, Patrick Canton, S.K.
Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba, Tonia Kandiero na Bisera
Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja mwishoni mwa hafla hiyo
Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa
TANESCO, Henry Kilasila, (kualia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269