.

WAZIRI WA AFYA ATHIBITISHA SERIKALI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA AFYA KWA MIAKA MITANO

Oct 7, 2016

Na Magreth Magosso, Kigoma

IMEFAHAMIKA kuwa,Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa dhati katika sekta ya afya ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vifaa na vifaa tiba ili kuzuia vifo vinavyozuilika ndani ya miaka mitano.

Akithibitisha kauli hiyo jana kigoma ujiji katika mkutano mkuu wa wauguzi nchini  waziri mwenye dhamana Ummy Mwalimu alisema mpaka sasa wizara imepunguza baadhi ya kero za vifaa akitolea mfano Hospitali ya taifa ya rufani ya Muhimbili ambapo kunamabadiliko ya utenadaji kazi kwa watumishi wa afya.
“mimi ni mwanamke nipo kwa ajili ya wanawake wajawazito katika kutaua kero zinazowakabili lakini msilalamike sana pale muuguzi anapohitaji mipira ya mikono kwa kuwa kuna wakati vituo vya afya na hospitali zetu hazina vifaa na vifaa tiba ,mchangie pale panapohitajika” alifafanua Mwalimu.
Alisema ili kukabiliana na hilo serikali imetenga fedha za kutosha kupunguza kero mtambukwa katika hospitali na vituo vya afya na zahanati kulingana na bajeti husika lakini serikali ina dhamira ya dhati kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,ili kuokoa uhai wa mama na mtoto.
Mwalimu alisema mpaka sasa mafanikio kwa baadhi ya magonjwa yameonekana hasa ugonjwa wa ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI), Maralia, lakini bado serikali inafanya jitihada za nguvu kuwekeza katika vifaa na vifaa tiba kwa miaka mitano kwa nia ya kuimarisha uchumi wa taifa hasa rasilimali watu ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Aidha aligusia changamoto ya uhaba wa  wauguzi nchini inakabiliwa kwa 48% hali inayomlazimu kila muguzi kuhudumia wagonjwa 1500 kwa siku ambapo kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) ilitoa mwongozo wa kuwa muguzi mmoja ahudumie wagonjwa 8 kwa siku, ili kuwapunguzia mchoko wa kazi.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Ummy Mwalimu Mkuu wa mkoa wa kigoma, Emanuel Maganga alisema kada ya uguzi ni sehemu ya maisha ya watu, serikali haina budi kutimiza mikakati yake katika kada hiyo, ambayo inakabiliwa na changamoto kadhaa ambapo zikitiliwa mkazo ustawi wa jamii utaimarika.
Mwisho.

--
Magreth Magosso
Jamboleo news paper
0757736863

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช