Jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya
Libya limetangaza kuwa, limefanikiwa kuwaangamiza wanachama 80 wa kundi
la kigaidi la Daesh katika mapigano yaliyotokea kwenye mji wa pwani wa
Sirte.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya
Libya imesema kuwa, jeshi hilo limefanikiwa kuwaangamiza wanachama
wasiopungua 80 wa kundi la kigaidi la Daesh waliokuwa wakitoroka kutoka
eneo moja la mji wa Sirte. Taarifa hiyo imesema askari wasiopungua 8 wa
Libya pia wameuawa katika mapigano hayo na wengine 57 wamejeruhiwa.
Tarehe 12 Mei jeshi la Libya lilianza operesheli kubwa iliyopewa jina
la al Bunyanul Marsus kwa shabaha ya kukomboa mji wa Sirte
unaodhibitiwa na kundi la Daesh. Wanachama wa kundi hilo waliukalia kwa
mabavu mji huo wa kaskazini mwa Libya mwezi Juni mwaka 2015.
Ripoti za hospitali za mji wa Sirte zinasema kuwa, zaidi ya askari
450 wanaoiunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya na wanachama
2500 wa kundi la Daesh wamekwishauawa hadi sasa katika operesheni hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269