Breaking News

Your Ad Spot

Oct 8, 2016

WAZIRI WA HABARI AFUNGA TAMASHA MBEYA

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kushot) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wakufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya  leo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni wakati  wa mkufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ( kulia) ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji Basata, Geodfrey Mngereza.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni wakati wa  kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ( kulia) ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji Basata, Geodfrey Mngereza.

Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya


Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.


Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.


“Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.


Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.


“Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa  ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.


Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages