NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
ABIRIA kutoka Vijiji
vilivyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika Mkoa
wa Kigoma wamebaki njia panda kuelekea kigoma mjini na wengine hawajui hatma ya
mizigo yao,baada ya basi walilokuwa wamepanda linalofanya shughuli
ya usafirishaji kutoka Sigunga kwenda Kigoma mjini la Saratoga kutumbukia katika mto ilagala uliopo wilaya ya Uvinza.
Akifafanua hilo Shuhuda wa ajali hiyo,Mwenyekiti wa SACCOS
Kijiji cha Ilagala Abdallah Mpolwe alisema wakiwa katika shughuli zao za
kawaida pembezoni mwa kivuko hicho,waliona kivuko cha Mv-Ilagala kikiwajibika,ilipotia
nanga ndipo basi hilo la abiria linalotoa huduma ya usafiri kutoka Sigunga
kwenda kigoma Mjini la Saratoga likitoka ndani ya kivuko hicho,lakini ghafla basi hilo lilirudi nyuma na kutumbukia mtoni.
Alisema Novemba ,23,
mwaka huu saa 2.30 asubuhi ndipo ajali hiyo ilitokea ambapo chanzo cha ajali ni kushindwa kwa breki la basi hilo lenye
uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 60,baada ya kushindwa kupandisha barabara kutoka ilipotia nanga
kivuko ,na nchi kavu na kukiri hakuna abiria aliyekufa japokuwa
inasemekana kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye alibaki humo kutokana na maradhi
aliyokuwa akiugua .
Kwa mujibu wa mmoja wa nahodha wa kivuko hicho jina hifadhini
kwa usalama wa mahusiano na wadau wa kivuko
hicho alisema baada ya kutia nanga ,dereva aliondoa basi katika kivuko hicho
kama kwaida yake lakini kwa bahati mbaya gari ilishindwa kupanda mlima wa
barabara husika hatimaye ilirudi kinyumenyume hatimaye kutumbukia mtoni huku dereva akiwa hai.
Jamboleo lilipiga hodi ofisini kwa Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui alipohojiwa juu ya ajali hiyo alisema wanasubiri utaratibu
kutoka kwa mmiliki wa mabasi ya Saratoga kwa ajili ya kwenda kijiji cha ilagala
katika kivuko cha mto huo kushuhudia uhalisia wa mambo na kuahidi kutoa tarifa
kamili baada ya kutoka katika eneo la tukio.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269