.

BOMBA JINGINE LA KUSAFIRISHA MAFUTA LARIPULIWA NIGER DELTA NCHINI NIGERIA

Nov 28, 2016

Waasi wa eneo la kusini mwa Nigeria la Niger Delta wameshambulia kwa kuripua bomba jingine la kusafirisha mafuta katika eneo hilo.
Paul Etaiga, afisa wa eneo la Ughelli katika jimbo la Niger Delta ametangaza kuwa hujuma dhidi ya bomba la mafuta ilifanywa hapo jana.
Kundi linalojiita Walipizaji Kisasi wa Niger Delta ambalo limeshambulia mara kadhaa vinu na mabomba ya mafuta katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa nishati hiyo limeshadidisha mashambulio yake hayo katika miezi ya karibuni.
Wanamgambo wa kundi la Walipizaji Kisasi wa Niger Delta
Mafuta yanachangia asilimia 70 ya pato la taifa la Nigeria ambapo tangu mwezi Agosti mwaka huu uchumi wa nchi hiyo umezorota kutokana na mashambulio na hujuma hizo na kushuka kwa bei ya mafuta.
Na hii ni katika hali ambayo kukithiri idadi ya vijana wasio na ajira na kutoshughulikia viongozi wa eneo la Niger Delta matakwa ya vijana hao kumezusha manung'uniko ya kijamii na uasi wa ubebaji silaha katika eneo hilo.../

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช