.

MUUNGANO UNAOONGOZWA NA MAREKANI UMEUA RAIA WASIO NA HATIA WA IRAQ

Nov 28, 2016

Raia wasiopungua 18 wameuliwa katika eneo la makaazi ya raia la mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq katika shambulio lililofanywa na muungano unaoongozwa na Marekai kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi nchini humo.
Duru moja ya Iraq imetangaza kuwa watu 18 wakiwemo wanawake 14 wameuawa katika shambulio la ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Marekani katika eneo la al-Ba'ath mjini  Mosul makao makuu ya mkoa wa Neinawa.
Mauaji ya wanafunzi mjini Mosul na shambulio dhidi ya hafla ya maombolezo katika eneo la Daquq, mjini Kirkuk lililosababisha kuuawa raia 25 wakiwemo wanawake 15 ni miongoni mwa hujuma za karibuni zilizofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq na kunyamaziwa kimya na Umoja wa Mataifa.
Ndege za kivita za Marekani
Maafisa wa jeshi la Marekani wanadai kuwa huwalenga raia wa Iraq kimakosa, madai ambayo hayawezi kutetewa kwa kuzingatia ramani zilizopo za operesheni za kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwenye makucha ya kundi la kigaidi na kitakfiiri la Daesh na kujulikana wazi ngome za kundi hilo la kigaidi.
Mnamo mwezi Septemba mwaka 2014, muungano eti wa kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani ulianzisha mashambulio ya anga ndani ya ardhi za Syria na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kundi hilo la kigaidi na kitakfiri.../

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช