.

DC: MLINDOKO WAJAWAZITO ACHENI DAWA ZA ASILI KUONGEZA UCHUNGU MKOANI- KIGOMA

Nov 22, 2016

                                                                                     
NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA. 

RAI imetolewa kwa wanawake wajawazito wasitumie dawa za asili za kuongeza uchungu katika harakati za kujifungua  kwa kuwa inahatarisha uhai wa mama  na mtoto ,badala yake wafike mapema  katika vituo vya afya ili kuokoa maisha yao.
                                    
Akitoa rai hiyo mbele ya ripota wa blog hii daktari mfawidhi wa kituo cha Afya cha  Nguruka  Dkt. Stanford- Chamgeni, kwa niaba ya  mkuu wa wilaya ya Halmashauri ya Uvinza  Mwamvua-Mrindoko wakati akikabidhiwa jengo la wazazi (maternity ward,) katika kijiji cha mganza kata ya mganza wilayani Uvinza,  ambalo limetolewa na Kanisa la POOL  OF SILOAM.

Naye  Kuhani Israel –Extra-Power, ambaye ni mwakilishi wa kiongozi mkuu wa kanisa hilo, alisema   hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kukamilisha huduma za kijamii hasa kuokoa maisha ya mama mjamzito na mtoto.

Kuhani Power, aliongeza kwa kusema  kuwa,  kusaidia maisha ya wenye uhitaji, lazima kuwepo na umoja kwa viongozi na jamii kwa ujumla  kwa kuwa Mungu hana upendeleo, kama kanisa nilazima  itoe huduma  kwa jamii.

Kwa upande wake,Ofisa mtendaji wa kata ya Mganza Bonifasi-Bahingai, amelishukuru kanisa hilo kwa kuwa wodi hiyo, itasaidia kutatua changamoto  ya uhaba uliokuwa ukikikabili kituo hicho  na kutoa wito kwa taasisi zingine za kidini kuona umuhim wa kusaidia huduma katika jamii.

 mmoja wa wananchi  wa kijiji hicho, Dafroza Gwimo alitanabaisha kuwa, uwepo  wa wodi hiyo itawarahisishia  kuondoa  changamoto iliyokuwepo  ya kwenda kujifungulia mbali,  na kupelekea kuhatarisha maisha ya mama mjamzito na mtoto.
Mwisho, 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª