Breaking News

Your Ad Spot

Nov 29, 2016

GPSA YAOKOA ZAIDI YA SH. BILIONI MOJA ZA SERIKALI KUPITIA MPANGO WA MANUNUZI YA PAMOJA

Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), imeokoa sh bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa GPSA, Jacob Kibona, amesema jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya sh. 58.1 kama kila taasisi ingenunua magari yake.

“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi ya pamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi hivyo unapaswa kupewa kipaumbele ili kuthibiti upotevu wa fedha kupitia,” Alisema Kibona.

Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya umma kama kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.

Kibona alisema katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka huu, GPSA imezikabidhi taasisi za serikali  magari  ya aina mbalimbali  yapatayo 136.

Alisema katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi, wamekuwa wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila inaposhindikana kutokana na sera za kampuni kubwa kuwa na mawakala wa usambazaji wamekuwa wakinunua kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum ya kupunguziwa bei.

Kibona alisema kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa mizigo kupitia bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya Sh. bilioni 62.7.

Alisema mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa taifa wa mawasiliano, vifaa vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara yaMaliasili na utalii.

Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka  huu pia walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali zikiwamo ndege mbili aina yaBombadier, zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada, vyote vikiwa na thamani ya Sh. bilioni 100.97.

Kibona  alisema GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi za serikali, kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa  karibu yote .

“Hata mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi, maghala yetu yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”

Alisema pi wana jukumu la kutoa huduma  ya mafuta kwa magari yaserikali na kwamba kwamba hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa mafuta kwa matumizi ya  ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea kupanuliwa ili uzifikie taasisi nyingi za umma.

Kibona alizishauri taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi kwa lengo la kutoa huduma bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma zinazopatikana zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages